WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO. BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni 22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2017,