Posts

Watuhumiwa wa ugaidi waigomea mahakama

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014. Wakizungumza leo mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao. Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa. Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi  hewa na mkuu wa upelelezi  kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake  wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi. Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifa...

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.PalamagambaKabudiakisikilizamaelezombalimbalialipokutananawatendajiwaWizaranaMahakamakatikaukumbiwamikutanoWizaranimjini Dodoma. ……………….. WaziriwaKatibanaSheriaProf.PalamagambaKabudiamewasilikatikaOfisizaMakaomakuuyaWizarazilizokondaniya Chuo Kikuu cha Dodoma nakulakiwanawatumishiwaWiza...

SAKATA LA RC PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS LAVUKA MIPAKA YA TANZANIA

Image
Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani. Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Asasi hizo zinazohusika na utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa habari zilikutana hivi karibuni mjini Kampala nchini Uganda katika mkutano uliokuwa ukizungumzia uhuru wa kujieleza na kupata habari. Tanzania kwenye mkutano huo iliwakilishwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) , miongoni mwa mijadala iliyotawala ni kukemea vitisho na vitendo vya kunyanyasa waandishi. Pia, wajumbe katika mkutano huo waligusia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli kwa kumtoa Nape Nnauye kwenye...

NAPE AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI MWAKYEMBE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwakaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitoa neno kwa Waziri mpya na Waziri aliyepita wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Mhe. Nape Moses Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akitoa shukurani zake kwa watendaji wa Wizara kwa muda wote aliotumikia Wizara katika makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe akimshukuru aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa kuitu...

Alicho andika Professor J baada ya wimbo wa Rais kuruhusu Wimbo wa Nay wa Mitego 0 BY CHOICETZ ON MARCH

Image
F

BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI AAGIZA NAYA WA MITEGO AACHIWE,NA WIMBO WAKE UPIGWE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa  Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego ’   baada ya kukamatwa juzi wilayani Mvomero mkoani Morogoro kisha kusafirishwa jana kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake wa WAPO alioutoa hivi karibuni hauna maadili na una maneno ya kichochezi. Akitoa agizo la Rais Magufuli,  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe   amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake aufanyie maboresho kwa kuongelea pia kuhusu wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi kisha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya habari. Aidha amesema kuwa, mara tu atakapoachiwa huru, Nay anapaswa kuonana na Waziri Mwakyembe ili ampe maelekezo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wimbo huo.

PICHA : NAY WA MITEGO AKIWA CENTRAL POLICE 0

Image

WAZIRI NCHEMBA ASEMA HAYA KUHUSU MTU ALIYEMTISHIA BASTOLA NAPE

Image
Baada ya tukio la mtu ana anayedaiwa kuwa ni Askari kanzu kuonekana akimtishia Bastola Waziri za zamani wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye  February 23, 2017 wakati alipotaka kuongea na Waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Wizara aliyokuwa akiiongoza.  Leo March 24, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, ya nchi Mwigulu Nchemba alitumia ukurasa wake wa Intagram na kusema..>>’ Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu ‘ ‘ Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiaskari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini ‘ – Mwigulu Nchemba ‘ Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sh...

MBUNGE HUSSEIN BASHE AMWANDIKIA UJUMBEE HUU NAPE NNAUYE

Image
Leo March 23, 2017 kumefanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Dkt. John Pombe Magufuli   amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria   Dkt. Harrison George Mwakyembe   kuongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa chini ya   Nape Nnauye . Baada ya mabadiliko hayo watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakilizungumzia hilo katika page zao za mitandao ya kijamii miongoni mwao ni Mbunge wa Nzega Mjini  Hussein Bashe   ambaye aliamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akimtaka Nape Nnauye kutovunjika moyo. Bashe ameandika>>> “Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It’s just beginning of a New journey.”   Follow Hussein M Bashe   @HusseinBashe Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It's just beginning of a New journey....

Maneno ya Waziri Nape mchana huu Kuhusu Ripoti ya Tukio la Makonda

Image
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye jana March 20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake. Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe. Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema ’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!‘

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WATEULE NCHINI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) leo tarehe 22 Machi, 2017 amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule 7 wanaowakilisha nchi zao nchini kutoka Hungary, Belarus, Guinea, Botswana, Niger, Cyprus na Bangladesh. Pichani Balozi Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Laszlo Eduard Mathe mwenye makazi yake Nairobi, Kenya.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Belarus nchini, Mhe. Dmitry Kuptel mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Balozi Mteule wa Guinea nchini Mhe. Sidibe Fatoumata KABA mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia mara baada ya kupokea Nakala zak...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BALAZA LA MAWAZIRI

Image

MBUNGE ZITTO KABWE AMPONGEZA KAMANDA TUNDU LISSU BAADA YA USHINDI WAKE

Image
CHAMA cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, kimempongeza Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kwa kushinda kiti cha urais wa Chama cha Wanasheria (TLS) katika uchaguzi uliofanyika juzi jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, alisema Lissu anastahili pongezi kwa kufanikiwa kushinda nafasi hiyo kutokana na changamoto zilizomkumba katika kuisaka. Alisema kuwa licha ya kupitia misukosuko mingi iliyokuwa inaonyesha njia ya kumkwamisha kufikia malengo yake, Lissu hakukata tamaa na alionyesha ujasiri. Mtemelwa alisema kupata nafasi hiyo kwa kiongozi kutoka upinzani ni dalili njema na kipimo kwa wapinzani na kwamba anapaswa kuitendea haki nafasi hiyo kwa ustawi wa vyama hivyo vya upinzani. “Mimi niseme tu kwamba, Lissu anastahili pongezi," Mtemelwa alisema. "Tunahitaji watu kama hawa, watu majasiri. Pamoja na kwamba ali...