Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) leo tarehe 22 Machi, 2017 amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule 7 wanaowakilisha nchi zao nchini kutoka Hungary, Belarus, Guinea, Botswana, Niger, Cyprus na Bangladesh. Pichani Balozi Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Laszlo Eduard Mathe mwenye makazi yake Nairobi, Kenya. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Belarus nchini, Mhe. Dmitry Kuptel mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Balozi Mteule wa Guinea nchini Mhe. Sidibe Fatoumata KABA mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia mara baada ya kupokea Nakala zake za Hati