MAYAI YA KUKU WA KISASA YADAIWA KUWA HATARI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mayai ya kuku wa kisasa yanayotengenezwa nchini yamedaiwa kuwa na mabaki ya dawa ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu. Akizungumza leo wakati alipozindua bodi mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu amesema amehakikishiwa na wataalamu hao kuwa dawa zinazotumika kwenye mayai na kuku hao zinabaki ambapo si salama kwa afya ya binadamu. Mwalimu amesema kutokana na dawa hizo kubaki kwenye mayai na kuku hao ameitaka TFDA kufanya utafiti ili kujua kiwango kipi cha dawa zilizopo ili Serikali iweze kuchukua hatua za haraka. “Hivyo tuwaachie TFDA waendelee na utafiti wao na wanapobaini ni kiasi gani cha dawa zilizomo kwenye mayai na kuku hao watuambie haraka dawa zipi hazitakiwi na zipi zinatakiwa ili kulinda soko la ndani,”amesema. Pia amewatahadhalisha wataalamu wa TFDA wasihofie kutoa majibu haraka kwa kufikiri kuwa watakwamisha soko la ndani hivy