MAYAI YA KUKU WA KISASA YADAIWA KUWA HATARI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mayai ya kuku wa kisasa
yanayotengenezwa nchini yamedaiwa kuwa na mabaki ya dawa ambazo ni
hatari kwa afya ya binadamu.
Akizungumza leo wakati alipozindua bodi
mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu
amesema amehakikishiwa na wataalamu hao kuwa dawa zinazotumika kwenye
mayai na kuku hao zinabaki ambapo si salama kwa afya ya binadamu.
Mwalimu amesema kutokana na dawa hizo
kubaki kwenye mayai na kuku hao ameitaka TFDA kufanya utafiti ili kujua
kiwango kipi cha dawa zilizopo ili Serikali iweze kuchukua hatua za
haraka.
“Hivyo tuwaachie TFDA waendelee na
utafiti wao na wanapobaini ni kiasi gani cha dawa zilizomo kwenye mayai
na kuku hao watuambie haraka dawa zipi hazitakiwi na zipi zinatakiwa ili
kulinda soko la ndani,”amesema.
Pia amewatahadhalisha wataalamu wa TFDA
wasihofie kutoa majibu haraka kwa kufikiri kuwa watakwamisha soko la
ndani hivyo wanatakiwa wawe wa kweli ili tatizo lililopo liweze
kupunguzwa.
Comments
Post a Comment