UHALISIA WA MSHAHARA WA MWALIMU BAADA YA MAKATO MAPYA YA 15% YA BODI YA MIKOPOYA ELIMU YA JUU




Baada ya bodi ya mikopo ya Elimu ya juu kufanyiwa makato haya ni baadhi ya mchanganuo wa makato kwa mshahara halisi,Baadhi ya makato katika mshahara wa Mwalimu ni kama inavyoonekana kwenye mabano;-

 Mfuko wa hifadhi ya jamii (35,800 sawa na asilimia 5%)

 Bima ya afya (21,480 sawa na asilimia 3% )

 CWT (14,320 sawa na asilimia 2%)

Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu -HESLB (107,400 sawa na asilimia 15 %)

 Income tax  (86,580 sawa na asilimia 12%).

Jumla ya Makato tu ni tsh 265,580/=.

Mwalimu anayelipwa mshahara wa  tsh 716,000/= anabakiwa na tsh.450,420/= kwa ajili ya kuchangia michango iliyowekwa kwa shuruti na kugharamia maisha yake.

*Kila mmoja apige hesabu kutokana na mshahara wake, bila kusahau kuweka makato ya mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali*

Baada ya hapo kinachobaki kipeleke kwenye matumizi yako binafsi:-

1. Maendeleo
2. Chakula
3. Kodi ya pango
4. Umeme
5. Maji
6. Usafiri
7. Mawasiliano
8. Shughuli za kijamii
9. Tegemezi
10.Michango ya mwenge, maabara, madawati nk.
11. Matibabu yasiyo kwenye bima.
12. Mavazi

Pamoja na makato hayo, hakuna;-

1. Posho ya usumbufu wala muda wa ziada.

2. Posho ya usafiri kwa wanaokaa mbali na kituo cha kazi kutokana na mazingira.

3. Posho ya makazi, nk.

Inamhitaji mwalimu kuwa mzalendo wa kupita kiasi, ama kuzuga, ama nidhamu ya woga katika kutekeleza majukumu yao.

Serikali, chama cha walimu CWT na vyama vyama vya wafanyakazi kwa ujumla embu oneni aibu juu ya hili.

Elimu haichezewi. 



NINI MAONI YAKO?Share nasi kwa kutoa maoni yako kupitia ukurasa wetu wa Facebook ambao ni *pharsblogspot*

Comments

Popular posts from this blog