STAA AGNES GERALD WAYA APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU,AACHIWA KWA DHAMANA
Mrembo
anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama
Masogange au Deal (28), amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia dawa za kulevya.
Mrembo
huyo anayeishi Makongo Juu ambaye alikuwa akitumia muda mwingi kujiziba
sura yake kwa mtandio na miwani ya Giza alisomewa tuhuma zake mbele ya
Hakimu Mkazi Willbard Mashauri. Hata hivyo, ameachiwa huru baada ya
kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.
Mahakama
ilimtaka Masogange kuwekwa dhamana ya milioni kumi hali kadhalika na
wadhamini wake wawili nao walitakiwa kuwekwa kiasi hicho cha fedha.
Aidha mahakama imemuamuru kutosafiri nje ya Dar ea Salaam bila ya kupata kibali cha Mahakama.Akisoma
hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa
kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika Eneo na Wilaya isiyojulikana
lakini ndani ya jiji la Dar es salaam, Masogange alitumia dawa za
kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Katika hatua ya pili, Mshtakiwa Masogange siku na mahali pasipojulikana alitumia dawa za kulevya aina ya OXazempam.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Masogange amekana kujihusisha na tuhuma hizo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu.
Mrembo
anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama
Masogange au Deal (28) akielekea kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu ambapo alisomewa Mashtaka ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu
kama Masogange au Deal (28)akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo jijini Dar es
Salaam.
Agnes
Masogange akitoka katika Mahakama hiyo akiwa na Wakili wake, Nictagon
Itege baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo ijini Dar es Salaam.
Agnes Masogange akiondoka katika Mahakamani
Comments
Post a Comment