Posts

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji asema Samatta anauwezo wa kucheza ligi kuu Uingereza

Image
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amekiri kuwa, mshambuliaji na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ana-ubora wa kucheza ligi kuu ya  England maarufu kama EPL. Shaffihdauda ilifanya juhudi za kumtafuta kocha huyo ambaye amewahi kufundisha soka England katika vilabu vya Wigan kabla haijashuka daraja pamoja na Everton kabla ya kupewa majukumu ya kuifundisha timu ya taifa ya Ubelgiji. Juhudi zilifanywa na Mbwana Samatta kuiunganisha shaffihdauda.co.tz na Martinez, hatimaye kocha huyo akatoa ushirikiano. Martinez amesema, Samatta ni mshambuliaji mwenye kiwango kikubwa na uwezo wa kucheza soka kwenye ligi yoyote ikiwemo EPL, pia amesema ameongea na kushauriana vitu vingi na Samagoal. Shaffihdauda.co.tz: Umeshawahi kumshuhudia Samatta akiwa uwanjani akiitumikia klabu yake ya Genk? Martinez: Mimi ni kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji kwa hiyo nafatilia kwa karibu sana ligi za hapa kwa hiyo nimeshamuona mara kadhaa akiwa uwanjani.

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA BLOGGER NA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR

Image
Pichani ni Mpendwa wetu Jennifer Livigha maarufu aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la CHINGA ONE  na Mwanachama mwanzilishi wa  Tanzania Bloggers Network  (TBN) enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake Kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.  Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer  Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama  Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer  Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Netwo

MREMBO RAY C AMLILIA MSANII WA WCB REYVANNY

Image
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ray C amedai kuwa anamkubali zaidi Rayvanny kutoka lebo ya WCB. Ray C amesema kuwa amesikia msanii huyo amewaandikia wasanii wengi nyimbo hivyo na yeye anatamani siku moja aje kufanya naye kazi. “Nampenda sana yule mtoto Rayvanny. Anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi,” Ray C amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. Mbali na hilo msanii huyo ameongeza kuwa anamheshimu sana Diamond Platnumz kutokana na kule alipofika kwakuwa muziki wake umefika sehemu ambayo wao hapo mwanzo hawakuwahi kufika.

AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aki

KINANA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA LEO

Image
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao . Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao . Wakienda eneo la kufanyia mazungumzo  Wakiwasili eneo la mazungumzo Ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM.  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 18, 2017. (Picha zote na Bashir Nkoromo) .

Uwoya ni Gusa Unate!

Image
DAR ES SALAAM: Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani)  anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kuachwa. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Uwoya aliyeomba hifadhi ya jila lake, staa huyo mwenye shepu na mvuto wa kudatisha kimahaba amekuwa akipapatikiwa sana na wan aume lakini mwisho wa siku huishia kuwaliza kwani yeye ndiye anayeamua kuendelea na wewe au akuache. “Uwoya namjua vizuri sana, yule ni hatari kwa wanaume. Kwanza anajijua kuwa ni mzuri hivyo amekuwa akiwadenguliwa wanaume wengi sana na orodha ya wanaomtokea kila siku ni kubwa. “Lakini akitokea kukupenda atakupenda kweli hadi unaweza kuona kero. Kwa kifupi anajua kupenda, kujali na kubembeleza kiasi kwamba ukinasa kwake ni vigumu kutoka ndiyo maana wapo wanaosema kwamba, Uwoya ni gusa unate! “Ila sasa, anaweza kukuchanganya kwa mahaba mazito lakini siku akiamua kukuacha, anaku