MREMBO RAY C AMLILIA MSANII WA WCB REYVANNY
Msanii
mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ray C
amedai kuwa anamkubali zaidi Rayvanny kutoka lebo ya WCB.
Ray
C amesema kuwa amesikia msanii huyo amewaandikia wasanii wengi nyimbo
hivyo na yeye anatamani siku moja aje kufanya naye kazi.
“Nampenda
sana yule mtoto Rayvanny. Anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia
wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi,” Ray C
amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mbali
na hilo msanii huyo ameongeza kuwa anamheshimu sana Diamond Platnumz
kutokana na kule alipofika kwakuwa muziki wake umefika sehemu ambayo wao
hapo mwanzo hawakuwahi kufika.
Comments
Post a Comment