Penzi la Jide, Nusu Bongo, Nusu Nigeria
Mpenzi wa Jide, Spicy naye akifunguka mbele ya kamera za Global TV Online. BAADA ya kukaa muda mrefu bila kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash, hivi karibuni mwanamuziki nguli wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ aliamua kumuanika mchana kweupe mpenzi wake mwingine aitwaye Spicy. Mwanamuziki huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, siku hizi za usoni baada ya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria, ameonekana ni mtu mwenye furaha na asiyeweza kuficha hisia zake za mapenzi ya kweli kwa mwenza wake huyo. Mapema wiki hii, Jide aliibuka ndani ya mjengo wa Global Publishers akiwa ameambatana na Spicy, mambo yakawa hivi mbele ya waandishi wa Global TV. Wapenzi hao wakifurahia jambo wakati wa mahojiano na Global TV Online. Amefika na je hakuna machozi tena? “Unajua hata kama nilikuwa naimba nyimbo nyingi zinahusiana na mambo ya kutendwa kimapenzi lakini ukweli nil