Penzi la Jide, Nusu Bongo, Nusu Nigeria


jide-na-spice-global-tv-online-2
Mpenzi wa Jide, Spicy naye akifunguka mbele ya kamera za Global TV Online.
BAADA ya kukaa muda mrefu bila kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash, hivi karibuni mwanamuziki nguli wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ aliamua kumuanika mchana kweupe mpenzi wake mwingine aitwaye Spicy.
Mwanamuziki huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, siku hizi za usoni baada ya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria, ameonekana ni mtu mwenye furaha na asiyeweza kuficha hisia zake za mapenzi ya kweli kwa mwenza wake huyo.
Mapema wiki hii, Jide aliibuka ndani ya mjengo wa Global Publishers akiwa ameambatana na Spicy, mambo yakawa hivi mbele ya waandishi wa Global TV.
jide-na-spice-global-tv-online-5
Wapenzi hao wakifurahia jambo wakati wa mahojiano na Global TV Online.
Amefika na je hakuna machozi tena?
“Unajua hata kama nilikuwa naimba nyimbo nyingi zinahusiana na mambo ya kutendwa kimapenzi lakini ukweli nilikuwa nafikisha ujumbe kwa jamii nzima, na pia kwa upande wangu siwezi kusema moja kwa moja sitaumizwa tena kwa sababu sijui ya mbeleni ila nafurahia nilipo sasa.
jide-na-spice-global-tv-online-7
Vipi penzi la Nigeria na Bongo linanoga?
“Hakuna shida kabisa kwa sababu mara nyingi nitakuwa kule na yeye atakuwa huku kwa kuwa sasa ni wapenzi kila kitu kinaweza kufanyika ili kudumisha penzi letu hilo hakuna shida na umbali siyo tatizo kwa watu wanaopendana.
Walikutanaje na Spicy na kuanzisha uhusiano?
“Unajua sisi ni wanamuziki na hivyo tulikutana katika mambo yetu ya muziki japokuwa tulikuwa na nia ya kufanya kazi pamoja na Mungu akaunganisha vitu vyake hapo.
jide-na-spice-global-tv-online-9Jide, Spicy katika picha ya pamoja na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.
Ana mpango gani zaidi mbeleni yeye na mpenzi wake?
“Tuna mipango mingi sana mizuri tumepanga na tunamuomba Mungu aikamilishe yote kama tulivyopanga na naamini atatusaidia sana.
Vipi kuhusu kipindi chake cha The Diary?
“Kipindi kitarudi siku si nyingi na kitakuwa na vitu vingi vizuri na Spicy atakuwepo kwa sababu ameshakuwa ni mmoja katika maisha yangu ya kila siku na ninaamini kila mtu atakipenda hivyo mashabiki wangu wasikate tamaa, wakae mkao wa kula.
Anazungumziaje bendi yake ya Machozi bado ipo?
“Bendi ipo isipokuwa nimebadilisha ule utaratibu wa kupiga sehemu moja kwa sababu mashabiki kila siku wanapenda vitu vya tofauti na biashara ni ushindani hivyo nimekuwa nazunguka na bendi yangu ili wale wa mikoani waliokuwa wanakosa burudani yangu wataipata na hivi sasa inaitwa The Band.
Anazungumzia ishu ya kuwahi kujiandalia kaburi lake na kuliposti mitandaoni?
“Unajua kila mtu ana imani yake ya dini na pia kufanya hivyo sidhani kama ni shida kwa sababu kutofanya na kufanya hivyo mwisho wa siku lazima mtu atakufa tu.
jide-na-spice-global-tv-online-6   Jide ns Spicy wakipata selfie na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.
Anazungumziaje Ray C, na mikakati ya kumsaidia?
“Unajua jukumu la kumsaidia Ray C siyo la kwangu peke yangu kama Lady Jaydee ila mimi namuombea na nina imani atakuwa vizuri tu kama alivyokuwa zamani na kwa pamoja tunaweza kumsaidia.
Yuko tayari kufanya kolabo na Ray C?
“Mimi sina shida niko tayari hata akiniamsha usingizini, siyo kwa Ray C tu mtu yeyote nafanya naye kolabo.
Ni kweli wamemalizana na Redio Clouds?
“Yameisha hakuna tatizo kama wao walivyosema pia.
Mahakama ilimuamuru amuombe radhi Ruge baada ya kesi kuisha, ameshafanya hivyo?
“Wao walishasema wamesamehe na yameisha sasa sioni sababu ya mimi tena kufanya kitu.
Ruge alikaririwa kuwa yupo tayari kupiga ngoma za Jide, je, yupo tayari?
“Nilishalijibu hilo (Global Tv haijawahi kuyasikia, kuyaona majibu yake) hivyo huwezi kumsikiliza yeye tu ukawa hujasikia kile nilichokijibu mimi. Tafuta kile nilichokijibu na mimi.
Kuna wimbo aliouandaa na mpenzi wake huyo?
“Ndiyo! Ila wimbo ni wa Spicy lakini tumeimba pamoja unaitwa Together na unazungumzia watu wawili wanaopendana. Unatoka Jumanne hii (iliyopita).
Alijisikiaje kunyakua Tuzo za EATV?
“Najisikia vizuri sana na pia natoa shukurani kwa mashabiki wangu kwa sababu ni jambo zuri na jema.
Anazungumziaje muziki wa Bongo kwa sasa?
“Kwa kweli muziki unakua siku hadi siku ni jambo la kujipongeza.”
Kwenye mahojiano hayo, Spicy naye alifunguka kuwa anampenda Jide, atakuwa anaishi Bongo kwa muda, Jide naye vivyo hivyo ataishi Nigeria kwa muda wakati wakiendelea kukuza muziki wao katika anga la kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog