Magari ya Mwalimu Nyerere Kivutio Kikubwa Makumbusho ya Taifa
DAR ES SALAAM: NI kumbukumbuku na historia ya aina yake kwa taifa letu! Yale magari aliyokuwa akiyatumia Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa nyakati tofauti wakati akiwa hai, yaliyopo kwenye Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Dalaam, yamefanywa kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani, wa nje na kuwasaidia wanafunzi hapa nchini kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu historia ya nchi yetu. Wanafunzi wakitazama magari aliyokuwa akiyatumia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambaragae Nyerere enzi za uhai wake. Gari aina ya Austin morris a 40 Austin morris a 40 Van Guard. Gari aina ya Mercedez Benz 230. Gari aina ya Mrolls Royce Phantom v2. Gari aina ya Rolls Royce 2 Mercedez Benz e 300 alilotumia hadi mwaka 1999 alipofariki dunia. Magari hayo yamepangwa kulingana na miaka ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa akiyatumia, kuanzia wakati wa ukoloni, wakati anashika madaraka mwaka 1961 na wakat