Magari ya Mwalimu Nyerere Kivutio Kikubwa Makumbusho ya Taifa
DAR ES SALAAM: NI kumbukumbuku
na historia ya aina yake kwa taifa letu! Yale magari aliyokuwa
akiyatumia Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa nyakati tofauti
wakati akiwa hai, yaliyopo kwenye Makumbusho ya Taifa jijini Dar es
Dalaam, yamefanywa kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani, wa nje na
kuwasaidia wanafunzi hapa nchini kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu
historia ya nchi yetu.
Wanafunzi wakitazama magari aliyokuwa akiyatumia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambaragae Nyerere enzi za uhai wake.
Magari hayo yamepangwa kulingana na
miaka ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa akiyatumia, kuanzia wakati wa
ukoloni, wakati anashika madaraka mwaka 1961 na wakati wote wa uongozi
wake hadi kifo chake, mwaka 1999.
Kamera yetu iliwashuhudia baadhi ya
wanafunzi wa Jiji la Dar wakiambatana na walimu wao katika eneo hilo la
Makumbusho ya Taifa wajikijifunza mambo mbalimbali kupitia magari hayo
aliyoyatumia Mwalimu Nyerere kwa nyakati tofauti.
Comments
Post a Comment