Sitta Azikwa Nyumbani Kwao Urambo Tabora
Wananchi wa Urambo wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta.
Staa wa Bongo Movie Iren Uwoya akiwa msibani.
… Kikundi cha wasanii kikiongozwa na Dude kikitumbuiza msibani.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Sitta likishushwa kwenye gari ili kupelekwa eneo la makaburi kwa ajili ya mazishi.
Jesneza likishushwa baada ya kufikishwa makaburini.
Jeneza lenye likiandaliwa kushushwa kaburini kwa mashine maalum.
Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk Alex Malasusa (mwenye kofia kushoto) akiwaongoza maaskofu, wachungaji, waumini na waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa, watoto wa marehemu, ndugu na marafiki wa marehemu wakiweka udongo kaburini.
Mjane wa Marehemu Sitta, Bi. Magreth Sitta akiweka shada kwenye kaburi la mumewe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe, Mohammed Aboud Mohmamed akiweka shada kwenye kaburi la marehemu Sitta.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiweka shada kwenye kaburi la marehemu Sitta.
Spika wa Bunge Mstaafu, Mama Anne Makinda akiweka shada kwenye kaburi la marehemu Sitta.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), freeman Mbowe akiweka shada kwenye kaburi la marehemu Sitta.
Spika wa Bunge, Tulia Ackson akiweka shada kwenye kaburi la marehemu Sitta.
URAMBO, TABORA: Aliyekuwa Spika wa
Bunge, Samuel Sitta leo amezikwa mjini Urambo. Mazishi hayo yaliongozwa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitoa neno la faraja kwa wafiwa,
marafiki na viongozi wa serikali. Mazishi hayo yalihudhuriwa na
mawaziri, wabunge na wananchi mbalimbali wakiwemo wasanii wa filamu na
muziki.
Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Elikael Mbowe naye alihudhuria na alikuwa
mmoja wa viongozi waliotoa hotuba katika msiba huo.
Mara baada ya mwili wa marehemu
kushushwa kaburini, viongozi mbalimbali wakiongozwa na waziri mkuu
pamoja na wana familia waliweka mashada ya maua kwenye kaburi hilo kisha
kikosi cha jeshi la polisi kilipiga risasi hewani kama heshima kwa
kiongozi huyo aliyeaga dunia Novemba saba mwaka huu nchini Ujerumani.SOURCE:GPL
Comments
Post a Comment