MZ Yakanusha Taarifa za Kifo cha Balozi Omar Ramadhan Mapuri

balozi-omar-ramadhan-mapuri
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia.
Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata chembe ya ukweli, Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri.
mapuri-hosp
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokwenda kumjulia hali Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Omar Ramadhan Mapuri katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. 
Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambaye kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika.
mapuri-hosp-2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akimpa pole Mhe. Mapuri aliyekuwa Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu.
Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao  ya kijamii, taarifa hizi siyo za kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.
Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali.
Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO
Zanzibar

Comments

Popular posts from this blog