Posts

Fanya hivi ili kuweka mvuto wa maandishi kwenye WhatsAppYako.

Image
WATU wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida, aidha, mtindo wake huwa mmoja. Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough? Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako. Kuweka bold Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota. Kwa mfano, ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold Kuweka italiki Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Ukiandika _italics_ itatokea ikiwa italics Kuweka strikethrough Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, u

Hii ndiyo familia ya Donald Trump

Image
Barron Trump Ndiye mwana wa pekee wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump na mke wake wa sasa, Melania. Ingawa alijitokeza katika mikutano kadha ya kampeni, kijana huyo wa miaka 10 hakuwa akionyeshwa mara kwa mara hadharani. Anapendelea kucheza gofu na baba yake, pia ana uwezo mkubwa wa kuzungumza Kislovenia kwa ufasaha. Melania Trump Ni mwanamitindo wa zamani, mzaliwa wa Slovenia, aliolewa na Donald Trump Januari 2005. Alijitokeza na kumtetea mumewe, baada ya kanda ya video kutolewa wakati wa kampeni na kumuonesha akijitapa kuhusu kuwadhalilisha kimapenzi wanawake. Julai 2016, aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa hotuba katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, baada ya Trump kuidhinishwa kuwania urais, ambapo alituhumiwa kuchukua maneno mengi kutoka katika hotuba iliyotolewa na Michelle Obama mwaka 2008. Alipoulizwa na CNN Oktoba ni jambo gani angetaka kubadilisha kwa mumewe, alijibu: “Kuandika

Clinton Aitupia Lawama FBI kwa Kushindwa Urais

Image
Aliyekuwa mgombea urais nchini Marekani kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton, amesema kushindwa kwake ghafla katika uchaguzi uliopita, kulichangiwa sana na hatua ya Mkurugenzi wa Shirika la Kijesusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi mpya wa sakata la barua pepe dhidi yake siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika. Bi. Clinton aliyepata kura za wajumbe 228 huku mpinzani wake Donald Trump akishinda kwa kura za wajumbe 290 amewaambia wafadhili wa chama chake kuwa hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini zake licha ya uchunguzi huo kutomkuta na hatia.

KUTANA NA MWANAMKE WA AJABU,ANAZUNGUSHA MWILI KAMA KAMBA,ANAKULA KWA MIGUU,ANATEMBEA KWA MIKONO

Image
 Kwa jina unaweza muita Leilani Franco(Backbend)  ana uraia wa nchi mbili (Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi umbali wa 20m  katika muda wadk  10.05  katika  tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, tarehe 11 Machi 2013.   Backbend binadamu ambaye ana uwezo wa kutembealea mikono na miguu kwa umbali mrefu.  Pia kama inavyodhaniwa kwa kawaida Mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine,  lakini kwa mwanamke huyu imekuwa ni tofauti kabisa, Mwanamke huyu ana uwezo wa kutumia miguu yake  katika shughuli zake binafsi kama Kula na kadhalika.....  Hatimaye, Leilani pia anashikilia rekodi ya Dunia kutokana na uwezo wake katika kuuzungusha  Mwili wake.

MZ Yakanusha Taarifa za Kifo cha Balozi Omar Ramadhan Mapuri

Image
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia. Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata chembe ya ukweli, Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokwenda kumjulia hali Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Omar Ramadhan Mapuri katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.  Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambaye kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed

Sitta Azikwa Nyumbani Kwao Urambo Tabora

Image
Wananchi wa Urambo wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta. Staa wa Bongo Movie Iren Uwoya akiwa msibani. Kulwa Kikumbi ‘Dude’ akiwa msibani Urambo pamoja na waombolezaji wengine. …Waombolezaji wakiendelea na ibada wakati   … Kikundi cha wasanii kikiongozwa na Dude kikitumbuiza msibani. Wenyeji wa Urambo wakiwa msibani, wanasikiliza nasaha mbalimbali za viongozi. Spika wa Bunge, Job Ndugai (kwenye nembo) akiwaongoza wabunge msibani. Jeneza lenye mwili wa marehemu Sitta likishushwa kwenye gari ili kupelekwa eneo la makaburi kwa ajili ya mazishi. Jesneza likishushwa baada ya kufikishwa makaburini. Jeneza lenye likiandaliwa kushushwa kaburini kwa mashine maalum. Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk Alex Malasusa (mwenye kofia kushoto) akiwaongoza maaskofu, wachungaji, waumini na waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi. Viongozi

BREAKING NEWZ:Askari Ajipiga Risasi Kifuani, Afariki Dunia!

Image
MTWARA: Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, aliyetambulika kwa jina la PC Sengerama amefariki dunia baada ya kudaiwa kujipiga risasi ya moto kifuani leo majira ya alfajiri wilayani Tandahimba mkoani humo. Inadaiwa kuwa wakati askari huyo anafanya hivyo alikuwa katika lindo kwenye Benki ya NMB, Tandahimba.   Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari la polisi. Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwambambe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema bado hawajafahamu chanzo cha askari huyo kujiua. “Ni kweli kama mlivyosikia, askari huyo amefariki dunia alfajiri ya leo kwa kujipiga risasi, lakini bado hatujafahamu nini chanzo cha kujiua. “Jeshi la Polisi linaendelea uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo, taarifa zikipatikana zenye ufasaha tutawaambia,” amesema Kamanda Mwambambe. Taarifa zingine zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kupelekwa nyumbani kwao mkoani Mwa

MAMA NA MWANA WAJIFUNGUA WATOTO KUTOKA KWA BABA MMOJA NA MWEZI MMOJA.

Image
Mama na mwana wakiwa wamebeba watoto wao Mama na mwana wajaliwa kupata watoto kwa mwezi mmoja na kwa baba mmoja. Mwanamke kutoka Afrika Kusini, Mildred Mashego na binti yake Patricia, wameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mama wa kwanza na binti wa kuzaa kupata watoto kwa mwezi mmoja na kwa baba mmoja. Pia wote wawili wamejaliwa kupata watoto wa kiume huku Patricia akimtangulia mama yake siku nne kujifungua

Aunt Ezekiel Ateketeza Laki Sita Kwa Picha (Zicheki Hapa)

Image
Staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel (28), pamoja na mzazi mwenzie Moses Iyobo (22) wakiwa katika pozi. Aunt Ezekiel na Moses Iyobo wakiwa na mtoto wao Cookie.   Wakiwa katika matembezi. staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mtoto wake Cookie. Mahaba niue. Wakiendelea kujiachia ndani ya maji. Aunt Ezekiel na Moses Iyobo wakifanya yao. Cookie akifanya yake. Cookie akiwa amelala na mama yake. Aunt Ezekiel akijiachia na mtoto wake. HIVI karibuni kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, habari ya mjini ilikuwa ni staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel (28), pamoja na mzazi mwenzie Moses Iyobo (22), kutokana na picha zao mbalimbali walizokuwa wamezitupia wakiwa pamoja na mtoto wao, Cookie. Staa huyo aliyeolewa na mfanyabishara Sunday Demonte kisha jamaa huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya Uarabuni,  baadaye Aunt alimkabidhi Iyobo moyo wake na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja. Katika kuelekea siku ambayo Aunt amezal