Posts

Sitta Azikwa Nyumbani Kwao Urambo Tabora

Image
Wananchi wa Urambo wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta. Staa wa Bongo Movie Iren Uwoya akiwa msibani. Kulwa Kikumbi ‘Dude’ akiwa msibani Urambo pamoja na waombolezaji wengine. …Waombolezaji wakiendelea na ibada wakati   … Kikundi cha wasanii kikiongozwa na Dude kikitumbuiza msibani. Wenyeji wa Urambo wakiwa msibani, wanasikiliza nasaha mbalimbali za viongozi. Spika wa Bunge, Job Ndugai (kwenye nembo) akiwaongoza wabunge msibani. Jeneza lenye mwili wa marehemu Sitta likishushwa kwenye gari ili kupelekwa eneo la makaburi kwa ajili ya mazishi. Jesneza likishushwa baada ya kufikishwa makaburini. Jeneza lenye likiandaliwa kushushwa kaburini kwa mashine maalum. Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk Alex Malasusa (mwenye kofia kushoto) akiwaongoza maaskofu, wachungaji, waumini na waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi. ...

BREAKING NEWZ:Askari Ajipiga Risasi Kifuani, Afariki Dunia!

Image
MTWARA: Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, aliyetambulika kwa jina la PC Sengerama amefariki dunia baada ya kudaiwa kujipiga risasi ya moto kifuani leo majira ya alfajiri wilayani Tandahimba mkoani humo. Inadaiwa kuwa wakati askari huyo anafanya hivyo alikuwa katika lindo kwenye Benki ya NMB, Tandahimba.   Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari la polisi. Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwambambe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema bado hawajafahamu chanzo cha askari huyo kujiua. “Ni kweli kama mlivyosikia, askari huyo amefariki dunia alfajiri ya leo kwa kujipiga risasi, lakini bado hatujafahamu nini chanzo cha kujiua. “Jeshi la Polisi linaendelea uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo, taarifa zikipatikana zenye ufasaha tutawaambia,” amesema Kamanda Mwambambe. Taarifa zingine zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kupelekwa nyumbani kwao mkoani...

MAMA NA MWANA WAJIFUNGUA WATOTO KUTOKA KWA BABA MMOJA NA MWEZI MMOJA.

Image
Mama na mwana wakiwa wamebeba watoto wao Mama na mwana wajaliwa kupata watoto kwa mwezi mmoja na kwa baba mmoja. Mwanamke kutoka Afrika Kusini, Mildred Mashego na binti yake Patricia, wameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mama wa kwanza na binti wa kuzaa kupata watoto kwa mwezi mmoja na kwa baba mmoja. Pia wote wawili wamejaliwa kupata watoto wa kiume huku Patricia akimtangulia mama yake siku nne kujifungua

Aunt Ezekiel Ateketeza Laki Sita Kwa Picha (Zicheki Hapa)

Image
Staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel (28), pamoja na mzazi mwenzie Moses Iyobo (22) wakiwa katika pozi. Aunt Ezekiel na Moses Iyobo wakiwa na mtoto wao Cookie.   Wakiwa katika matembezi. staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mtoto wake Cookie. Mahaba niue. Wakiendelea kujiachia ndani ya maji. Aunt Ezekiel na Moses Iyobo wakifanya yao. Cookie akifanya yake. Cookie akiwa amelala na mama yake. Aunt Ezekiel akijiachia na mtoto wake. HIVI karibuni kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, habari ya mjini ilikuwa ni staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel (28), pamoja na mzazi mwenzie Moses Iyobo (22), kutokana na picha zao mbalimbali walizokuwa wamezitupia wakiwa pamoja na mtoto wao, Cookie. Staa huyo aliyeolewa na mfanyabishara Sunday Demonte kisha jamaa huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya Uarabuni,  baadaye Aunt alimkabidhi Iyobo moyo wake na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja. Katika kuelekea siku ambayo Au...

Chombo Kisichotambulika Chaanguka Kutoka Angani

Image
Kifaa kikubwa chenye urefu wa mita 4.5 (futi 15) na upana wa mita 1.2 ambacho hakijatambulika kimeanguka kutoka angani Kaskazini mwa Myanmar. Kifaa hicho kiliapatikana juzi Alhamisi na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo ambao mpaka sasa bado hawajaweza kutambua kama ni kifaa gani. Pia kifaa kingine kilianguka juu ya paa kikiwa na maandishi ya Kichina takribani wakati mmoja na hicho kingine licha ya kutoleta madhara yeyote. Watafiti wa mambo ya anga wameeleza kuwa huenda kifaa hicho ni  mabaki ya satellite iliyorushwa na China mnamo March 11 kutokea kituo cha  Jiuquan Satellite Launch Centre ili kufanya tafiti za anga.

Chombo Kisichotambulika Chaanguka Kutoka Angani

Image
Kifaa kikubwa chenye urefu wa mita 4.5 (futi 15) na upana wa mita 1.2 ambacho hakijatambulika kimeanguka kutoka angani Kaskazini mwa Myanmar. Kifaa hicho kiliapatikana juzi Alhamisi na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo ambao mpaka sasa bado hawajaweza kutambua kama ni kifaa gani. Pia kifaa kingine kilianguka juu ya paa kikiwa na maandishi ya Kichina takribani wakati mmoja na hicho kingine licha ya kutoleta madhara yeyote. Watafiti wa mambo ya anga wameeleza kuwa huenda kifaa hicho ni  mabaki ya satellite iliyorushwa na China mnamo March 11 kutokea kituo cha  Jiuquan Satellite Launch Centre ili kufanya tafiti za anga.

Kambi Kubwa ya Jeshi la Marekani Yashambuliwa, Wanne Wauawa

Image
Bagram: Watu wanne wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa baada ya Wanamgambo wa Taliban kuishambulia Kambi Kubwa ya Jeshi la Marekani ya Bagram nchini Afghanistan. Jeshi linaloongozwa na NATO, limesema kuwa shambulizi hilo ni la kujitoa muhanga kwani mlipuaji huyo alivalia bomu bila wao kujua aliwadanganya kuwa nyeye ni miongoni mwa wafanyakazi wa kambi hiyo, wakati wafanyakazi walipokuwa wakiwasili katika kambi hiyo kwa shughuli za siku. Kundi la Taliban linasema kuwa ndilo lilihusika. Hakuna taarifa zaidi kuhusu uraia wa wale waliouawa.