Chombo Kisichotambulika Chaanguka Kutoka Angani
Kifaa
kikubwa chenye urefu wa mita 4.5 (futi 15) na upana wa mita 1.2 ambacho
hakijatambulika kimeanguka kutoka angani Kaskazini mwa Myanmar.
Kifaa hicho kiliapatikana juzi Alhamisi
na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo ambao mpaka sasa bado
hawajaweza kutambua kama ni kifaa gani.
Pia kifaa kingine kilianguka juu ya paa
kikiwa na maandishi ya Kichina takribani wakati mmoja na hicho kingine
licha ya kutoleta madhara yeyote.
Watafiti wa mambo ya anga wameeleza kuwa
huenda kifaa hicho ni mabaki ya satellite iliyorushwa na China mnamo
March 11 kutokea kituo cha Jiuquan Satellite Launch Centre ili kufanya
tafiti za anga.
Comments
Post a Comment