Posts

Aveva Amuandikia Barua Rais Magufuli Ya Kuomba Radhi

Image
Rais wa timu ya Simba, Evans Aveva. UONGOZI wa Klabu ya Simba umemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, ukiomba radhi kwa kitendo cha mashabiki wao kufanya uharibifu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Wakati barua hiyo ikiwasilishwa serikalini, upande wa pili Simba chini ya rais wake, Evans Aveva, imeteua kamati maalum ya wajumbe wenye uwezo mzuri wa kifedha kwa ajili ya kuiwezesha kufanya vizuri msimu huu, kamati ambayo ilianza kazi kuanzia katika mechi dhidi ya Yanga. Sehemu ya viti vilivyog’olewa na mashabiki wa Simba siku ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga. Kabla hujaijua kamati hiyo, upande wa kuomba radhi ni kuwa hatua hiyo imefikiwa siku chache tangu serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwakilishwa na waziri wake, Nape Nnauye kuzisimamisha Simba na Yanga kuutumia uwanja huo baada ya uharibifu kutokea wakati wa mechi baina ya timu hizo, Jumamosi iliyopita. Rais wa Jamhuri ya Muung

ZIARA YA JAJI MKUU WA AUSTRALIA YA KUSINI NCHINI TANZANIA

Image
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto) akisoma kitabu kinachohusu Chama cha Majaji Wanawake Tanzania wakati alipotembelea ofisini kwa Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman. Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika ofisi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, iliyopo kwenye jengo la Mahakama ya Rufani Tanzania, jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Kourakis yupo nchini kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kujenga ushirikiano katika utendaji kazi wa Mahakama baina ya nchi hizo mbili. Kushoto ni Bi. Emma Gorman, Katibu wa Jaji Mkuu wa Australia Kusini.

Madaktari Wasema Said Ally Hatoona Tena

Image
Said Ally akiwa katika hali ya huzuni baada ya kuambiwa haotoona tena. …akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Paul Makonda. …Akizungumza na Mhe. Makonda. Mapema leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally aliyetobolewa macho na Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena. Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema: “Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote. “Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake. “Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia

TANESCO YATILIANA SAINI MIKATABA YA KUJENGA NJIA YA UMEME WA KILOVOTI 400 UTAKAOUNGAMISHA MIJI YA SINGIDA, ARUSHA NA NAMANGA NCHINI KENYA

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani 309.26  Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo  Mhandisi Mramba, (kushoto), na  S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba

Kizza Besigye Azuiwa Kutoka Nje Ya Nyumba Yake

Image
Kizza Besigye akizungumza na ofisa wa polisi. KAMPALA: Mwanasiasa wa siku nyingi nchini Uganda, Kizza Besigye leo amezuiliwa na polisi wa Kayihura kutoka nje ya nyumba yake.   …Baada ya kushuka garini. Polisi hao wamemweleza mwanasiasa huyo kwamba wamepewa amri kutoka juu kwamba haruhusiwi kutoka nje ya nyumba yake. …Polisi wakiwa wameweka kizuizi. Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa Twitter mwanasiasa huyo ameandika: “ Happening just now, Kayihura Police officers say their orders are not to allow me out of my home at all- period! Impunity at its highest.” Na Leonard Msigwa/MTANDAO.

PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini

Image
Kama wewe unadhani huna fedha, basi kuna wengine ambao wamezichimbia ardhini, tena kwa mamilioni. Benki ya chini ya ardhi iliyosheheni mamilioni ya fedha, zilizoswekwa ndani ya mifuko myeusi ya plastiki na kufukiwa mchangani, imechimbuliwa na matrekta ya kutengeneza barabara jijini Arusha huku noti nyekundu zikitawanywa kila kona na kufanyika kuwa 'Sadakalawe - Amina,' kwa kila mpita njia ambaye angeweza kujitwalia fungu. Ilikuwa ni mshikemshike katika eneo la Mianzini mjini Arusha , ambako kuna mradi mkubwa wa upanuzi wa barabara ya kutoka Mianzini Mataa hadi Ilkiding'a unaoendelea. Watu walipigana vikumbo katika harakati za kujineemesha na fedha zilizokuwa zimetapakaa eneo hilo. Ikiwa imesheheni noti tupu, tena nyekundu na mpya, kufumuliwa kwa akaunti hiyo ya benki ya chini ya ardhi pamoja na kuwa neema kwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo, kuligeuka pia kuwa kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo, Christopher Akoonay

Magufuli Amwandalia Dhifa Ya Taifa Kabila

Image
 Rais John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar.  Kabila akimwamkia rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi  Ikulu katika dhifa ya taifa.  …Akimsalimia Mama Sitti Mwinyi, mke wa Ali Hassan Mwinyi.  …Akisalimiana na spika mstaafu  Anne Makinda .     …Akisalimiana na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid.   Sehemu ya waliohudhuria dhifa ya taifa.  Kuoka kushoto ni rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi.  Sehemu ya wageni waalikwa.  Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Raymond Tshibanda