Madaktari Wasema Said Ally Hatoona Tena



Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake.
“Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja.”
Na Hilaly Daud/ GPL.
Comments
Post a Comment