Shoga: tui la nazi lazima lionjwe!
SHOGA yangu u hali gani? Ni siku nyingine tena tulivu imefika na tumekutana kwenye kona yetu hii inayowaelimisha wengi hususan wanawake wenzangu japo wanaume nao siwaachi nyuma. Natumai na wewe ni mzima wa afya na kama mgonjwa nakuombea kwa Mwenyezi Mungu atakutia nguvu. Baada ya hayo tugeukie basi kwenye hiki kilichonifanya niwaandikie, si mnakumbuka mara ya mwisho nilitoa somo la chakula cha usiku hakifunikiwi! Wengi mlinipigia simu na kunitumia meseji jinsi mnavyowafanyia waume zenu. Inanipa raha sana kuona mada imewaingia kisawasawa na kuyafanyia kazi shoga, mwanamke sharti ujue kukipika chakula bwana! Kiwe kitamu pia usimfunikie mume wako eti kwa kuhofia nzi au kupoa, kifunue ili akila ajihisi ameridhika, upo? Shoga baada ya hayo, nimepata maswali mengine mengi kutoka kwa nyie wasomaji wangu wengi mnaniuliza hivi tui la nazi lina utamu gani? Wengine mnauliza kwani lazima lionjwe? Jamani hata hili kweli la kuuliza au la kujiongeza mwenyewe? Umeshaandaa m