Ndege mpya ya serikali yatua Dar
Ndege mpya ya serikali,
Bombardier Q400 ikiwa katika Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
baada ya kuwasili nchini mchana wa leo kutoka Canada.
Ndege hiyo ikimwagiwa maji mara baada ya kutua.
Rubani aliyeileta ndege hiyo akiwa katika pozi baada ya kutua.
Baadhi ya watu walioipokea ndege hiyo wakiwa ndani wakifurahia mandhari yake.
Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Ndege la ATCL wakikagua ndege hiyo.
Marubani waliyeileta ndege hiyo na kiongozi mmoja wa ATCL wakiwa katika picha ya pamoja.
Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizoagizwa na serikali, aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada tayari imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Ndege hizi mbili zimenunuliwaili kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa sasa lina ndege mbili, ambayo moja ni ya kukodi.
Ujio wa ndege hizi mbili umeelezwa kuwa umelenga kusaidia katika soko la ndani na kurahisisha usafiri wa anga kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Ndege hizi zitakuwa na uwezo wa kutua katika viwanja vingi nchini kwani huhitaji takribani barabara ya urefu wa kilomita 1 tu kuweza kuruka tofauti na ndege zinazotumia injini ya jet ambazo huhitaji zaidi ya barabara yenye urefu wa kilomita 2 kuweza kuruka.
Comments
Post a Comment