Shoga: tui la nazi lazima lionjwe!
SHOGA
yangu u hali gani? Ni siku nyingine tena tulivu imefika na
tumekutana kwenye kona yetu hii inayowaelimisha wengi hususan wanawake
wenzangu japo wanaume nao siwaachi nyuma. Natumai na wewe ni mzima wa
afya na kama mgonjwa nakuombea kwa Mwenyezi Mungu atakutia nguvu.
Baada ya hayo tugeukie basi kwenye hiki
kilichonifanya niwaandikie, si mnakumbuka mara ya mwisho nilitoa somo la
chakula cha usiku hakifunikiwi!
Wengi mlinipigia simu na kunitumia
meseji jinsi mnavyowafanyia waume zenu. Inanipa raha sana kuona mada
imewaingia kisawasawa na kuyafanyia kazi shoga, mwanamke sharti ujue
kukipika chakula bwana!
Kiwe kitamu pia usimfunikie mume wako eti kwa kuhofia nzi au kupoa, kifunue ili akila ajihisi ameridhika, upo?
Shoga baada ya hayo, nimepata maswali
mengine mengi kutoka kwa nyie wasomaji wangu wengi mnaniuliza hivi tui
la nazi lina utamu gani? Wengine mnauliza kwani lazima lionjwe? Jamani
hata hili kweli la kuuliza au la kujiongeza mwenyewe? Umeshaandaa mboga
yako, nazi ukune mwenyewe, machicha ukamue mwenyewe eti kuonja unataka
usaidiwe. Tui la nazi sharti lionjwe shoga, usiwe zoba utaibiwa mjini,
ahii!
Wengine wanaishia kuonja machicha tu,
wanashindwa kumalizia kupata utamu wa tui lenyewe, wanashindwa kujua
hata tui la kwanza na la pili lipi tamu. Nikupashe tu shoga, wanaume wa
sasa ni wa kimjinimjini, wakizunguzungu tena wengine wakichinachina!
Chunga sana siku hizi kwani wanawake
wengine wanaweza kumnasa mwandani wako na wakamuandalia tui, balaa
itakuja kama tui hilo litakuwa zito kuliko unalopika wewe, mume akiona
hilo ni tamu anaweza kukuhama. Wengi wazembe wamewahi kukimbiwa na waume
au wapenzi wao kutokana na kupika tui jepesi na kutokuwa na ladha!
Unapoandaa tui la nazi yako jitahidi
liwe nzito na likolee kwelikweli na hata mume au mpenzi wako anapokuja
kula basi asiione lina matatizo au jepesi, mfanye awe analitamani kila
siku kwani usipofanya hivyo na wenzako nje wakamtengenezea na akakosea
kulila, ndiyo mwanzo wa kuhama kwenye jiko lako.
Uzuri wa mwanamke siyo sura tu bali hata
katika mapishi kwenye jiko lenye kiwanja cha sita kwa sita. Ukiwa
jikoni humo jitahidi kupika mboga, ukiamini kwamba ukitia tui, mumeo au
mchumba wako hatabanduka na kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine.
Tumewahi kushuhudia wanawake wengi wakilalamika kuchukuliwa kwa waume
wao au wapenzi wao au wachumba wao na wanawake wengine kisa ni jinsi
wanavyowatayarishia tui na kila wakila wanaona ni hovyo tu.
Ubaya ni kwamba siku hizi wasichana
wengi hawafundwi kama zamani ambapo walikuwa wakikusanyika wanawake watu
wazima na kuwafundisha wasichana jinsi ya kutengeneza tui zito
litakalomfanya mume asihangaike na mboga za nje.
Siku hizi wasichana wanaona mambo hayo
kuwa ni ya kizamani na wala hawana haja ya kufuatilia kwa wanawake
waliowapita umri ambao wameona mengi, hivyo kubaki kuharibu tui na
kutotamanika. Ukiwa wa bush kwenye miti mikavu na vichaka unaachwa, sasa
kwa nini usijifunze hata kwa kuibia kwa wenzako?
Shoga, acha nikupe kaubuyu kadogo!
Wenzako wakipewa jembe kabla hawajaingia shambani wanaangalia kwanza
kama wataweza kulilimia, halijaharibika!
Wanalichukuwa na kuingia shambani,
wakimaliza kulima wanachukuwa nazi na kuanza kukuna, wanahakikisha
wanapata machicha ya kutosha, wanakamua hadi tui lile zito walione
likitoka! Wakionja huo utamu wake, mwanaume hatoki! Kwanza akafuate nini
huko nje?
Uzuri wa siku hizi tui la nazi hata
ukilila kwa chakula cha usiku tamu, chakula cha mchana tamu. Ukilila
kipindi cha baridi tamu, kipindi cha joto tamu. Ukilila kwa kufunika
chakula tamu, ukikifunua napo tamu.
Ukilila kwa kuimba nyimbo zote tamu, iwe Mchiriku au Taarab linakuwa tamu.
Shoga najua umenipata, basi yafanyie kazi niliyokuambia ili ndoa yako idumu.
Kwa leo sina mengi tuonane wiki ijayo! Kwa ushauri, nitumie meseji tu kwa namba yangu hapo juu nitajibu
Comments
Post a Comment