Posts

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AWATAKA ASKARI WA USALAMA BARABARANI KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA AJALI KWA KUFUATA SHERIA

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akieleka ukumbi wa mkutano wakati wa kikao alichofanya na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Askari Polisi hao ni wadau muhimu katika kufanikisha Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa amesimama wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani(hwapo pichani), wakiimba wimbo wa maadili wa Jeshi la Polisi. Kushoto ni Naibu Inspekta

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 06.08.2016

Image
Posted by JAFE MALIBENEKE at Saturday, August 06, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Pinterest

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR.

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa   kukagua uzalishaji  wa sukari katika kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.   Kulia ni  mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif .  Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera,  Ashuwin  Rana baada ya kuwasili kwenye  kiwanda  cha sukari cha Mtibwa  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif  Ali Seif .   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipokitembelea kiwanda hich

Jide, Mwarabu wazua utata

Image
STORI: MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na Mwarabu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, wamezua utata wa aina yake kufuatia msanii huyo ‘kumposti’ mara kwa mara kwenye mtandao wake wa Instagram. Risasi Jumamosi lilianza kumfuatilia Jide baada ya kutonywa na chanzo kuwa msanii huyo amekuwa akimposti Mwarabu huyo na kwamba kuna kila dalili ni mtu wake aliyerithi mikoba ya aliyekuwa mumewe, Gardner Habash.   “Nyie kama vipi fuatilieni kwa makini kwenye Instagram yake, mtagundua tu ukweli, kuna kitu maana hata akimposti huyo jamaa huwa anaweka maneno yenye utata, hataki kufunguka moja kwa moja kama ni mpenzi wake au vipi,” kilisema chanzo hicho. Baada ya chanzo hicho kulitonya Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Jide na kuziona picha tofauti zikimuonesha akiwa amekaa na Mwarabu huyo huku akisindikiza na ujumbe ambao hautoi majibu ya moja kwa moja kama ni mtu wake au la. Alip

RC MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU) UKONGA JIJINI DAR LEO

Image
-Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu . -Awaahidi kuwapatia Ambulance  -Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi.  Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)ukonga Jijini Dar na amezungumza mengi moja kubwa nao ni Mhe. Makonda amewaeleza kuwa hakuna wafanyakazi wazalendo kama Askari kwani wao wako tayari kufa ili taifa letu Liwe salama. Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa.  Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake al

Taarifa za ndani ya familia… Diamond ‘mchafu’

Image
Diamond Platnumz Imelda Mtema na Musa Mateja Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’. Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn.   Zari. ILIKUWAJE? Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna kiumbe. Lynn LYNN NAYE Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taarifa

Ray C full kicheko

Image
MSANII mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya aliye katika majaribu makubwa ya matumizi ya madawa ya kulevya, hivi sasa anadaiwa kuwa full kicheko kufuatia mabadiliko makubwa ya afya yake tangu alipoanza kupata matibabu katika kituo cha wahanga wa ‘sembe’, Sober House kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani. Kwa mujibu wa bosi wa kituo hicho, Karim Bhanji, Ray C hivi sasa yupo vizuri tofauti na zamani na kwamba kwa jinsi anavyoendelea, hali yake inazidi kutengemaa. “Unajua tatizo kubwa kwa Ray C ilikuwa kwamba alikuwa anapatiwa matibabu bila uangalizi wa kutosha. Ingawa alikuwa akinywa dawa, lakini kilichokuwa kinatokea ni kuwa anakwenda Mwananyamala kunywa dawa halafu anarudi nyumbani, huko mtaani anakutana tena na watu walewale anaendelea kutumia. “Lakini kwa kuja hapa, baada ya dawa anadhibitiwa, hatoki hivyo hapati nafasi ya kujaribu tena kutumia unga, nina imani hali yake itaimarika kadiri muda unavyoenda,” alisema Bhanji na kuongeza kuwa akiwa kituoni, Ray C amesh

Tundu Lissu Akamatwa na Polisi… Msigwa Ahutubia Iringa

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi, Singida. Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake. Kukamatwa kwa Lissu  Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. ” Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

Wabunge 3 kesi ya rushwa mil.30/- waachiwa

Image
Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibala. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewaachia huru wabunge watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 30. Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage aliwaachia huru washitakiwa hao baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwasilisha hati ya kuwafutia mashitaka. Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Mhe. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mhe.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa, Mhe.Victor Mwambalaswa. Wabunge hao na majimbo yao katika mabano ni Kangi Lugola wa Mwibara mkoani Mara maarufu kama ‘Nyoka wa Shaba,’ Suleiman Saddiq ‘Murad’ (Mvomero – Morogoro) na Victor Mwambalaswa (Lupa – Songwe). Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi akisaidiwa na Wakili Emmanuel Jacob kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imetajwa kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali. Kishenyi alidai

MCHUNGAJI AFARIKI BAADA YA KUFUNGA SIKU 30 AKITAKA KUVUNJA REKODI YA YESU

Image
AFRIKA KUSINI: Mchungaji mmoja amefariki baada ya kufunga usiku na mchana siku 30 akitaka kuvunja rekodi ya Yesu aliyefunga kwa siku 40. Mchungaji huyo aliondoka nyumbani kwake na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka nia kwa Mungu ya kujitenga na anasa za ulimwengu.

Breaking News: Evans Aveva akamatwa na Takukuru, pesa za Okwi zatajwa

Image
Rais wa Klaabu ya Simba, Evans Aveva anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru). Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi. Habari za uhakika zinaeleza, Aveva amekamatwa jana na amelala katika moja ya vituo vya polisi jijini Dar es Salaam. Saa chache baada ya Evans Aveva kushikiliwa na Takukuru, kumeibuka sababu kadhaa ambazo zinazungumzwa kuwa ni chanzo. Kumekuwa na taarifa ambazo si rasmi kuwa Aveva aliingiza fedha za Okwi zaidi ya Sh milioni 450 kwenye akaunti yake binafsi kuhofia zichukuliwe na TRA kwa kuwa Simba inadaiwa. Simba inadaiwa zaidi ya Sh milioni 650, hali hiyo imesababisha kuonekana kama vile alikuwa akikwepa kodi. Malipo ya fedha hizo, zaidi ya Sh milioni 450 ni malipo ya ununuzi wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambazo Simba ilimuuza katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Taarifa hizo zimeeleza kwamba waliamua kuzificha ili waweze kujenga uw