Posts

JE, UNA HERUFI M KATIKA KIGANJA CHAKO? HII NDIO MAANA YAKE

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama 'M' katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya 'M' basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu

Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996

Image
Meli ya MV Bukoba ikwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama. KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 20 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu. Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama. Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu. Mnara wa Kumb

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

Image
Mh. Charles Kitwanga aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.  “Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.  Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.  “Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.  Waziri

Tanzia: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Wilson Kabwe Afariki Dunia

Image
  Marehemu Wilson Kabwe. ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amefariki usiku wa kuamkia leo nchini India alikokuwa ameenda kutibiwa. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Rais John Pombe Magufuli, Aprili 19 alimsimamisha kazi Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  pesa zaidi ya bilioni 3. Rais Magufuli alichukukua uamuzi huo siku ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo. Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe alikuwa ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye alih

A-Z Shoo ya Jide Mlimani City

Image
Malkia wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee usiku huu amefunika vilivyo katika shoo yake ya Nasimama Tena iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City. Staa huyo akiwa na vijana wake wamepiga shoo kali ya Live iliyochukua saa tatu na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki walioshindwa kujizuia kukaa kwenye viti vyao na kunyanyuka mara kwa mara kwenda stejini kucheza nyimbo mbalimbali za malkia huyo. Shoo hiyo imehudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Fleva na Bongo Movies wakiwemo Alikiba, Idrisa Sultan, Wema Sepetu, Elizabeth Michael na wengineo kibao. Usikose kuangalia Global TV Online kuona video za matukio yote yaliyojiri. Picha: Clarence Mulisa, Gabriel Ng’osha na Rishard Bukos / GPL

MATUKIO YA BUNGENI LEO.

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.   Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Patson Sobha(aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma walitembelea Bunge kama sehemu ya mafunzo jana mjini Dodoma.  Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Simanjirio Mhe. James Ole Milya(wa pili kushoto), Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe.John Heche(wa pili kulia) na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.  Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(kushoto) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge. Picha na Ti

Sakata la Mauaji Msikitini Mwanza: Kundi la Kigaidi la ISIS lahusishwa

Image
YADAIWA ni kisasi baada ya Polisi kuwakamata wanaharakati wa IS saa 24 kabla. "baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele, bendera hiyo ni kama ile inayotumiwa na kundi la kigaidi la IS" "Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga," "Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa," Habari za uhakika ambazo Nipashe imezipata zinasema. Imam huyo na wafuasi wake, waliuwawa na kundi la watu wanane waliokuwa na bu

SAKATA LA ESCROW, IPTL LAIBUKA UPYA BUNGENI

Image
Kambi ya upinzani imeliibua upya bungeni sakata la Escrow, Richmond na umiliki wa kampuni ya IPTL, huku ikihoji sababu za Rais John Magufuli kutoheshimu maazimio ya Bunge ya kumwajibisha Sospeter Muhongo, badala yake kumteua tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Hoja hizo ziliibuliwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika wakati akiwasilisha maoni ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17. Muhongo alikuwa akiiongoza wizara hiyo wakati kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo umeme kusubiri kumalizika kwa mzozo wa kimkataba baina ya kampuni ya IPTL, inayozalisha umeme na Shirika la Umeme (Tanesco). Bunge lilimuona Profesa Muhongo kuwa alishindwa kuwajibika na kusababisha Serikali kupoteza mapato. Profesa Muhongo alilazimika kujiuzulu wadhifa huo saa chache kabla ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwet

Msichana mwingine kati ya wale 276 waliotekwa na Boko Haram apatikana

Image
Baada ya miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana zaidi ya 276 wa shule na kupatikana kwa mmoja May 18 2016 msichana mwingine  Serah Luka  amepatikana kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno. Mkuu wa jeshi la polisi Nigeria ametibitisha taarifa hizo japo hakutoa maelezo mengine ya ziada.  Taarifa zimeripotiwa siku mbili baada ya kupatikana kwa msichana mwingine wa kundi hilo la Chibok girls Amina Ali . Amina Ali  ambaye alipatikana May 18 2016 alialikwa na Rais wa Nigeria nyumbani kwake akiwa pamoja na mama na mtoto wake aliyejifungua wakati akiwa mateka wa kundi la kigaidi la Boko Haram,  anasema kati ya wanafunzi wenzake, sita walipoteza maisha walipokua mateka.

KESSY AMVAA JOHN MNYIKA

Image
Jina la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge la Kumi na Moja na kuzua mvutano. Lowassa alitajwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), wakati akijibu hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliyekuwa akihoji na kuonesha kushangazwa na uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati alijiuzulu bungeni hapo baada ya kuelemewa na kashfa ya akaunti ya ‘Tegeta Escrow’. Akijibu hoja hizo, Keissy ambaye siku zote ni mbunge mwenye hoja machachari alimvaa Mnyika  na kuhoji mbona wao ( UKAWA) walimchukua  Lowassa na kumfanya  kuwa mgombea wao wa Urais  wakati alijiuzulu uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond. “Mnabeza  uteuzi wa Muhongo wakati Lowassa alivyojiuzulu hapa hapa bungeni mlimchukua mkamtembeza nchi nzima. Leo angekua Rais mgesema nini?"  Alihoji Keissy . Mnyika alikuwa alisoma hatuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Ni

DIAMOND PLATINUMS ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET . Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi Juni nchini Marekani. Mwananmuziki Diamond Platnumz ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act: Africa. Wakali wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Wizkid, Yemi, AKA na wengineo

Image
Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi Juni nchini Marekani. Mwananmuziki Diamond Platnumz ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act: Africa. Wakali wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Wizkid, Yemi, AKA na wengineo

Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

Image
Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini. Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta. Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu. “Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania. Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Sh

BREAKING NEWS: GARDNER AMJIBU LADY JAY DEE ,AGOMA KUOMBA RADHI HADHARANI

Image
Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo. Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ. Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso. Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani. Alisema

Ndege ya Mfalme Mswati Yazuiwa Canada

Image
Mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu akiwa na mmoja wa wake zake. NDEGE binafsi ya Mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu, imezuiwa nchini Canada kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili kutokana na mzozo wa deni. Ndege hiyo ilizuiwa kama sehemu ya kesi iliyo mahakamani, iliyowasilishwa na aliyekuwa mfanyibiashara mwenza wa mfalme Mswati raia wa Singapore Shanmuga Rethenam, ambaye anasema kuwa anaudai ufalme wa Swaziland kiasi cha dola milioni nane. Jana Jumatano msemaji wa serikali ya Swaziland Percy Simelane, alikana madai kuwa mfalme ana deni lolote na kuongeza kuwa hatasema zaidi kwa kuwa kesi iko mahakamani.

Wabongo Wataja Njia 3 za Kumaliza Sakata la Lugumi

Image
Rais John Pombe Magufuli. DAR ES SALAAM: Sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises inayomilikiwa na Said Lugumi (pichani) kudaiwa kuingia mkataba tata wa mabilioni ya shilingi wa kufunga mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini, limeingia mitaani huku baadhi ya Wabongo wakitaja njia 3 za kumaliza ishu hiyo. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walionesha shaka yao kuhusu sakata la Lugumi kuwa gumzo likiumiza vichwa vya wabunge kama vile mhusika amekwenda Ulaya, hivyo wakatoa maoni yao. Shida Waziri, mkazi wa Ubungo External, Dar alisema: “Lugumi mwenyewe tunaambiwa hayupo mbali, anaendelea kuishi kwa amani hapahapa Tanzania. Mimi nashauri aitwe, ahojiwe mbele ya jopo la watu maalum, wakiwemo Usalama wa Taifa. “Hii itasaidia sana kwani ataweza kuanika kila kitu. Mkataba ulivyokuwa, ulivyokwenda, nani na nani walihusika.” Said Lugumi John Joseph, mkazi wa Kigogo, Luhanga, Dar: “Mimi nashauri serika

Zari, mama Diamond…

Image
Zarinah Hassan ‘Zari’ DAR ES SALAAM: Inadaiwa ilitokea lakini haikuandikwa! Kuna habari kuwa, ile safari ya familia ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kula bata kwenye nchi za Ulaya, ilikuwa na mambo mengi lakini kubwa ni madai ya kuwepo kwa mtifuano kati ya mama Diamond, Sanura Kasim na Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenzake, Diamond. Kwa mujibu wa chanzo, mtifuano kati ya Zari na mkwewe huyo ulitokea baada ya siku moja mkwe huyo kuteleza kwenye ngazi za umeme wakiwa wanapanda, Zari akamuwahi kwa kumshika mkono hali iliyomtibua mama huyo. Diamond na mama yake mzazi, Sanura. “Jamani kuna hili la mama D (Diamond) na Zari kutibuana nchini Sweden. Wakiwa kule, siku moja walikuwa wakipanda zile ngazi za umeme, sasa mama Diamond akateleza, Zari akasema amuwahi ili mkwewe asifike chini, si akamchenjia. Aliusukuma mkono wa Zari na kumwambia amwache mwenyewe. “Naamini kuna kutokuelewana kwa ukweli kabisa kati ya mama Diamond, bintiye yu

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 19.05.2016

Image