Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996
Meli ya MV Bukoba ikwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama.
KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 20
iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na
Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV
Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37
ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza
ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.
Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga,
iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114
waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na
kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji
la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya
miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.
Mnara wa Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba uliopo Makaburi ya martehemu waliotokana na ajali hiyo, Igoma – Mwanza.
Hakika Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la
Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake
aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa
Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia
Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.
Mkoani Kagera.
Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979
ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika
Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo
30 kutoka ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza
maisha katika Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake
ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na
idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo
wa kubeba abiria 430).
Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21
Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo
iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo
walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara
nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
Wakati leo tunakumbuka tukio hili ambalo
limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo
imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio
usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri (Picha zote na Maktaba).
Lakini wakati tunatafakari suala hilo,
pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe bila kusubiri kusukumwa na mtu
hususani wale wenye mamlaka ya kuleta matokeo chanya katika kuboresha
hali ya usafiri majini Ikiwemo Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini
SUMATRA kwamba tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo ya
Mv.Bukoba?
Na Kama kuna jambo tulijifunza, je
tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya
uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia
sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu? Je,
tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa
na majanga ya majini au nchi kavu?.
Lakini pia wapo waliohoji na bado
wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo
ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado
wanaendelea kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea
tangu kuzama kwa meli hiyo? Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa
ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya Watanzania
ikiwemo ile ya mv Spice Ireland iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika
Mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja Zanzibar.
Lakini yote Tisa, Kumi ni stofahamu
iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa
nchini.Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Wakaguzi wa na Waangalizi kwa
maana ya Mamlaka husika, Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na
Timu yake na wapo waliosema chombo kilikuwa kibovu.
Wapo waliodai chombo hicho kilikuwa
kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria
wenyewe walisababisha ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda Melini
ilihali chombo kilikuwa kimejaa huku mlolongo huo ukihitimishwa na wale
waliohusisha ajali hiyo na Imani za Kishirikina.
Mimi nasema sina nia ya kuandika hayo
yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo
yote ili kila mmoja kwa namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna
ya kufanya ili kuepukana na ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine
husema tusiangalie tulipoanguka bali tuangalie tulipojikwaa.
Wapo wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na
marafiki zao na mmoja wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha
yake ni Mwanamitindo maarufu hapa nchini ambae pia anafanya shughuli
zake barani Ulaya Flavian Matata ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi
pamoja na binamu yake.
Pamoja na watu wengine, Matata amekuwa
na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa kufika Mkoani Mwanza katika eneo
la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza maisha katika ajali hiyo ya
Mv.Bukoba
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
Hakika inauma sana
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
Comments
Post a Comment