KESSY AMVAA JOHN MNYIKA
Jina
la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na
vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge
la Kumi na Moja na kuzua mvutano.
Lowassa
alitajwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), wakati
akijibu hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliyekuwa akihoji na
kuonesha kushangazwa na uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri
wa Nishati na Madini wakati alijiuzulu bungeni hapo baada ya kuelemewa
na kashfa ya akaunti ya ‘Tegeta Escrow’.
Akijibu
hoja hizo, Keissy ambaye siku zote ni mbunge mwenye hoja machachari
alimvaa Mnyika na kuhoji mbona wao ( UKAWA) walimchukua Lowassa na
kumfanya kuwa mgombea wao wa Urais wakati alijiuzulu uwaziri Mkuu kwa
kashfa ya Richmond.
“Mnabeza
uteuzi wa Muhongo wakati Lowassa alivyojiuzulu hapa hapa bungeni
mlimchukua mkamtembeza nchi nzima. Leo angekua Rais mgesema nini?" Alihoji Keissy .
Mnyika
alikuwa alisoma hatuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Nishati na
Madini ambayo ilikuwa ikiponda uteuzi wa Profesa Muhongo
Comments
Post a Comment