WAZIRI MKUU: SERIKALI ITAAGIZA TANI 70,000 ZA SUKARI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makazi yake jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano). Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati). “Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au m