LEICESTER CITY YAKABIDHIWA KOMBE LAO LA LIGI KUU ENGLAND
Leicester
City wamesherekea ubingwa wao wa Premier League ambao ni wa kwanza
katika historia ya klabu hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 132 iliyopita.
Furaha hiyo imechagizwa na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa King Power.
Leicester wamekabidhiwa rasmi ubingwa wao baada ya kujihakikishia kutwaa
taji hilo tangu siku ya Jumatatu wakati Tottenham iliposhindwa kuifunga
Chelsea.
Klabu hiyo imeandika historia ambayo imeuteka ulimwengu ambapo nahodha
Wes Morgan pamoja na kocha Claudia Ranieri kwa pamoja walinyanyua taji
la Premier League baada ya kumaliza safari ya kupambana kutoshuka daraja
hadi kutwaa ubingwa katika kipindi cha miezi 12.
Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton ulikuwa unaendelea kudhihirisha
uwezo, kujitoa na ubora uliowapa ubingwa, lakini siku ya Jumamosi ya May
7 ni zaidi ya mchezo wa soka kutokana na kufunikwa na hisia za kila
aina.
Comments
Post a Comment