WAZIRI MKUU: SERIKALI ITAAGIZA TANI 70,000 ZA SUKARI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makazi yake jijini Dar es salaam.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani
70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini
na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano).Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na
waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay
jijini Dar es Salaam.Akitoa
ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema
tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya
Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini)
na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).“Tani
nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke
bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia
Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa
mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri
Mkuu.Amesema
anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi
karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. “Mheshimiwa Rais ameagiza
watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia
tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza
uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.Amewataka
wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao
wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa
Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili
kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.Akifafanua
kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri
Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari
nchini linakwisha ifikapo 2019. “Wananchi wasiogope, Serikali imechukua
hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,”
alisema.“Tunao
mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa
ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo
matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.“Serikali
imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo,
Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari
na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza
kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.
Comments
Post a Comment