DUNIA INA MAMBO MAZITO BI HARUSI AMPA SUMU MUMEWE
Msichana
mdogo alieolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa
kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya
panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.
Kesi
hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema
kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa
kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.
Shahidi
wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa
msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi
katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru
huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya
alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke
aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi
zimekithiri.
Msichana
huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya
panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo
bwana Sani alifariki.
Alisema
kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia
mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u
aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa
sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana
Sani.Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.
Jaji
Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u
ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa
kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.
Ushahidi
wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa
Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani
ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim
Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho
kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande
vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula
vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini
hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee
aliyeendelea kula.
Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.
Lakini
alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine
watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.
Viongozi
wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua
watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya
mauaji.
Nigeria
haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo
taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la
kibinaadamu la
Comments
Post a Comment