Mambo 8 Muhimu Kuhusu Huduma Mpya ya WhatsApp
KUTOKANA na tatizo la kuingiliwa kwa mawasiliano ya watumiaji wa WhatsApp, hivi karibuni kampuni hiyo ilianzisha huduma ya end-to-end encryption ili kuboresha huduma zao za mawasiliano hasa katika nyanja ya kuimarisha ulinzi wa mawasiliano ya wateja wao. 1. End-to-end encryption ni nini? Hii ni huduma mpya ya WhatsApp inayotumiwa kwa ajili ya kulinda mawasiliano baina ya mtumaji na mpokeaji kwenye mtandao huo bila mtu wa kati kuingilia mawasiliano hayo. huduma hii pia inapatikana iwapo mtumianji wa ataingiza toleo jipya la WhatsApp. Inatumika kwenye simu zote za iOS na Android. 2. Unawezaje kuwezesha (activate ) huduma hii? Haya yote yanafanyika kwa mfumo kujiendesha wenyewe (automatically), hauhitaji kufanya mpangilio (setting) ili kuwezesha usiri wa mawasiliano yako. 3. Je, huduma hii pia inahusisha upigaji simu wa kwenye WhatsApp call? Ndiyo, kama meseji zako zinalindwa hata WhatsApp calls pia zinalindwa kwa mfumo ...