BOSI WA ZAMANI WA TRA HARRY KITILLYA, SHOSE SINARE NA SIOI SOLOMONI WANYIMWA DHAMANA
Kamishna
wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga
mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya
kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo
wamerejeshwa rumande.
Kitillya,
alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu
wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi
Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.
Dhamana
yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo
mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.
Dk.
Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi
ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili
Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.
Upande
wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa
haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya
ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.
Upande
wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi
hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya
Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama
hilo lakini alipewa dhamana.
Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.
Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mmoja
wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni
sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la
Magereza kwenda kwenye gari maalum, tayari kwa safari ya kurudishwa
rumande baada ya kesho yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.
Comments
Post a Comment