Mambo 8 Muhimu Kuhusu Huduma Mpya ya WhatsApp
KUTOKANA na tatizo la kuingiliwa kwa
mawasiliano ya watumiaji wa WhatsApp, hivi karibuni kampuni hiyo
ilianzisha huduma ya end-to-end encryption ili kuboresha huduma zao za
mawasiliano hasa katika nyanja ya kuimarisha ulinzi wa mawasiliano ya
wateja wao.
1. End-to-end encryption ni nini?
Hii ni huduma mpya ya WhatsApp
inayotumiwa kwa ajili ya kulinda mawasiliano baina ya mtumaji na
mpokeaji kwenye mtandao huo bila mtu wa kati kuingilia mawasiliano hayo.
huduma hii pia inapatikana iwapo mtumianji wa ataingiza toleo jipya
la WhatsApp. Inatumika kwenye simu zote za iOS na Android.
2. Unawezaje kuwezesha (activate ) huduma hii?
Haya yote yanafanyika kwa mfumo
kujiendesha wenyewe (automatically), hauhitaji kufanya mpangilio
(setting) ili kuwezesha usiri wa mawasiliano yako.
3. Je, huduma hii pia inahusisha upigaji simu wa kwenye WhatsApp call?
Ndiyo, kama meseji zako zinalindwa hata
WhatsApp calls pia zinalindwa kwa mfumo wa end-to-end encryption ambapo
mpigaji wa simu na mpokeaji ndiyo wataweza kuwasiliana wakati mtu wa
kati (third part) hatakuwa na uwezo wa kuona wala kusikia mawasiliano
hyo.
4. Vipi kuhusu midia?
Media zote ambazo ni video, audio, picha na mafaili pia yatakuwa na ulinzi kutoka kwa mtumaji kwenda kwa mpokeaji.
5. Vipi kuhusu Magrupu?
Group halitawekewa ulinzi mpaka ambapo mmoja kati ya members atakapokuwa na hiyo huduma yenye mfumo wa end-to-end encryption.
6. Utajuaje iwapo ujumbe/call yako imewekewa ulinzi?
WhatsApp inakupa uhuru wa kukagua iwapo
ujumbe/call yako kwenda kwa mpokeaji vitakuwa vimelindwa. Baada ya
kutuma ujumbe wako kwa mpokeaji, iwapo mawasiliano yako na mpokeaji wako
yatakuwa yamelindwa utapokea ujumbe huu “Messages that you send to this chat and cals are now secured with end-to-end encryption.”
Kutokea hapo, unaweza kuona QR code ambazo ni namba ambazo ni tarakimu
60. Pia unaweza ku-scan QR code yako na kuhakiki kwa kuifananisha na
zile tarakimu 60 za mtu unayewasiliana naye kwa wakati huo.
UJUMBE WENYEWE HUU HAPA
7. Ni kwa namna gani WhatsApp wameweza kufanikisha hivi?
WhatsApp wametumia ‘The Signal
Protocol’, iliyotengenezwa kwa Mfumo wa Open Whisper, kwa ajiri ya
ulinzi wa kimtandao (encryption). Lengo lake ikiwa ni kuzuia watu wa
kati (third paties) kuweza kuingilia mawasiliano hayo, mfano waharifu wa
kimtandao (cybercriminals) na serikali ili wasiweze kuingilia
mawasiliano binafsi.
8. Je, madhara yake ni nini kwa vyombo vya ulinzi?
Ulinzi huo utaleta changamoto kubwa
kwenye vyombo vya usalama(polisi) na sheria (mahakama) kiduni hasa
watakapotaka kuchunguza taarifa za matukio ya mtandaoni. Vyombo vya
usalama pamoja na wizara yenye dhamana ya mawasiliano kwenye nchi husika
ndiyo watakuwa na jukumu la kuhakikisha mawasiliano ya wananchi wao
yanakuwa yamelindwa kabla whuduma haijaruhusiwa nchini.
Comments
Post a Comment