Posts

WANAWAKE WA DODOMA WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGAMKIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA MANJANO FOUNDATION

Image
   Wanawake wa Mkoa wa Dodoma  wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara  na namna ya kuendesha Ujasiriamali Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma . Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika fursa hiyo na wanajulikana kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake hao kutoka Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa za ujasiriamali, changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa pamoja na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na kujua mbinu zipi watumie kujiwekea akiba.    Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser  Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo y

Kamati ya bunge wa miondombinu yatembelea miradi mbalimbali

Image
Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu yatembelea miradi mbalimbali inayotelezwa na taasisi zilizo chini ya kamati ambapo Mo Blog imekuandalia habari picha za jinsi ziara hiyo ilivyokuwa. Makamu Mwenyekiti wa Kamatiya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso (Mb), akisalimiana na uongozi wa Kampuni ya SMH Rail inayounda upya vichwa vya treni katika karakana ya reli iliyoko mkoani Morogoro, ambapo kamati hiyo iliyotembelea hivi karibuni kuona maendeleo ya uundwaji upya wa vichwa vya treni. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso (Mb) (wa pili kutoka kushoto), akipata maelezo ya namna kichwa kilichoundwa upya kinavyofanyakazi kutoka kwa mtaalam wa Kampuniya SMH Rail inayounda upya vichwa vya treni katika karakana ya reli iliyopo mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilitembelea karakana hiyo hi

SAKATA LA WASTARA KUPEWA TALAKA LACHUKUA SURA MPYA.WASTARA JUMA ATOROSHWA HOSPITALINI,

Image
Taarifa mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge, Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu. Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu. Wikienda lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa kwa jina la Abdulaziz Babu. Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina, jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi. Baada ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospita

Mkurugenzi wa Hanang asimamishwa akihusishwa na ubadhirifu wa Mil. 82

Image
Baraza maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara limewasimamisha kazi watumishi wanne wa Halmashauri hiyo, akiwemo mweka hazina wa Halmashauri hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara. Aidha katika maamuzi yake Baraza hilo pia limeazimia kwa kauli moja kwamba halina imani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Bwana Felix Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wa shilingi 82,873,000 na hivyo kupendekeza kwenye mamlaka zinazohusika kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazomkabili. Akifunga mkutano wa Baraza hilo maalumu,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bwana George Bajuta amewataja watumishi waliosimamishwakazi kuwa ni pamoja na mweka hazina wa Halmashauri Mazengo Matonya, mhasibu msaidizi Marseli

Baada ya Timu ya Taifa ya Chad Kujitoa AFCON 2017, Haya ndio Maamuzi ya CAF......

Image
Jumatatu ya March 28 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa inajiandaa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa nne wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Chad, habari zilizotoka March 27 kutoka shirikisho la soka Afrika CAF ni kuwa Chad wamejitoa. Baada ya Chad kujitoa kwa sababu za kutokuwa vizuri kiuchumi, CAF wamekumbushia sheria iliyowekwa January 15 2015, inaeleza kuwa kundi lolote litakalo salia na timu tatu, halitakuwa na best looser na badala yake kinara wa kundi ndio atakuwa anafuzu michuano hiyo pekee. Kwa sheria za CAF michezo ya Chad inafutwa na msimamo wa Kundi G unabakia kuongozwa na Misri kwa point 4, Nigeria point 2 na Tanzania kubakia mkiani kwa kuwa na point moja, ikumbukwe kuwa Taifa Stars ilicheza na Chad March 23 N’Djamena na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Penny azimia ndani ya gari, ala mzinga

Image
Muonekano wa gari hilo baada ya kugongwa. Stori:  Imelda Mtema, Wikienda Dar es Salaam: Bidada yamemkuta! Mtangazaji wa Zuku TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ amekumbwa na mkasa mwingine baada ya gari lake kupigwa mzinga maeneo ya Mikocheni jijini Dar, kwa kile kinachodaiwa alizimia barabarani kutokana na tatizo la ini linalomsumbua kwa sasa. Chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio hilo kilisema kuwa staa huyo alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Mark X kwa mwendo wa kawaida lakini akaanza kupunguza spidi taratatibu kutokana na maumivu yaliyompata ghafla na kusababisha bodaboda kugonga gari lake kwa nyuma. Mashuhuda wakiwa kwenye tukio. Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa, wakati tukio hilo linatokea ilikuwa mchana kweupe bodaboda nusura wamfanyizie. Pamoja na watu kusogelea kwenye tukio, Penny aliendelea kukaa ndani ya gari akiwa amejilaza hadi alipopata nafuu ndipo akaanza kuondoa gari taratibu. Wikienda lilipozungumza na Penny alisema alipatwa na hali hiyo

SAKATA LA RAY C KURUDI KWENYE MADAWA YA KULEVYA JIPYA LAIBUKA,ANASWA LIVE

Image
Stori: Musa Mateja, WikiendaLICHA ya kutumia nguvu nyingi kukanusha habari zinazochapishwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuwa, amerejea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenaswa ‘laivu’ akiwa ‘ameangusha gari’ kando ya barabara, habari ndiyo hiyo! Ray C ambaye kila anapoandikwa na Magazeti ya Global kuhusu kurejea kwenye unga, amekuwa akimtupia shutuma Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo kwamba anamchafua, alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni maeneo ya Mwananyamala Magengeni, Dar akiwa amezima yeye na mwanaume aliyekuwa naye hali iliyompa urahisi paparazi wetu kuwafotoa picha za kutosha. ISHU ILIANZA JANUARI Januari mwaka huu, gazeti hili liliripoti habari iliyokuwa na kichwa; CHIMBO LA UNGA LA RAY C LAGUNDULIKA. Baada ya habari hiyo kutoka, Ray C aliikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema: “Seriously kwa kweli huwa naumia sanasana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuniharibia j

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA PASAKA KANISA LA KKKT LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mchungaji Charles Mzinga alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Magufuli wakishiriki na waumini wengine Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. Kwaya wakati wa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini h

Fahamu aina saba za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke

Image
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke na kusababisha maumivu kwao lakini aina hizi saba ndiyo huonekana sana kwa wanawake wengi ambazo ni kama ifuatavyo:  I. Follicular cyst :  Ni uvimbe ambao hutokea wakati Ovulation isipotokea au baada ya Corpus Luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya Ovulation. Maumivu haya huonekana kwa robo ya wanawake wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa. 2.Corpus Luteum cyst ;  Ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida Corpus Luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwingine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Uvimbe huu huonekana kwen

Clouds media wamtembelea Chid Benzi Bagamoyo

Image
Wanafamilia wa ‪#‎CloudsMediaGroup‬ kutoka katika vipindi vya ‪#‎PowerBreakFast‬ ‪#‎Clouds360‬ na ‪#‎Harakati‬ wametembelea kituo cha Life &hope Rehabilitation centre "Bagamoyo" mahali ambapo Rapa Chidy Benz anapatiwa matibabu, wameongea na watumiaji sugu wa madawa ya kulevya ambao wanapatiwa matibabu katika kituo hicho kuhusu uzoefu wao hapo. Inategemewa kuwa Chidy Benz itamchukua siku 90 kuondoa madawa katika mwili wake na miezi 6 kumaliza matibabu yake kabisa. Pia wamewatakia sikukuu njema ndugu zetu hao.

Baba Diamond Ashinda Njaa

Image
NA WAANDISHI WETU, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia  shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi. Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma. Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya. TUJIUNGE NA CHANZO Chanzo makini kililiambia gazeti h