WANAWAKE WA DODOMA WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGAMKIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA MANJANO FOUNDATION
Wanawake
wa Mkoa wa Dodoma wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers
wakikisikiliza kwa Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara na namna ya
kuendesha Ujasiriamali Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma .
Mafunzo
ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano
yameanza mkoani Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika
fursa hiyo na wanajulikana kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo
yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake hao kutoka
Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa za ujasiriamali,
changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa pamoja na
nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia
washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na
kujua mbinu zipi watumie kujiwekea akiba.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano
Foundation Mama Shekha Nasser Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo
ya Ujasirimali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma..
Awamu
ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi
hasa "Make-Up Artistry". Awamu hii hapa washiriki watajua matumizi yenye
ueledi (professional) wa kutunza ngozi, kutumia vipodozi na namna ya
kuwapamba maharusi na wakazi wa Dodoma na maeneo jirani kwa kutumia
vipodozi sahihi na salama. Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata
fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la
kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita
katika kujiajiri katika tasnia ya vipodozi.
Mafunzo
haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na
Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi Pendwa vya LuvTouch Manjano.
Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake Zaidi ya 150
Kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Visiwani Zanzibar. Baadhi ya
washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Dodoma wameishukuru Taasisi ya
Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mradi huo.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa Dododma.
Wakieleza
zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa
wanawake wenzao wa mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar
kunufaika na mradi huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana
mafunzo hayo. Wakiendelea zaidi wamesema wapo tayari kupigana na
kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea
kipato kupitia kazi ya mikono yao
Comments
Post a Comment