Mkurugenzi wa Hanang asimamishwa akihusishwa na ubadhirifu wa Mil. 82
Baraza
maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara
limewasimamisha kazi watumishi wanne wa Halmashauri hiyo, akiwemo mweka
hazina wa Halmashauri hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara.
Aidha
katika maamuzi yake Baraza hilo pia limeazimia kwa kauli moja kwamba
halina imani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Bwana Felix
Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 wa shilingi 82,873,000 na hivyo kupendekeza kwenye mamlaka
zinazohusika kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi zaidi
wa tuhuma zinazomkabili.
Akifunga
mkutano wa Baraza hilo maalumu,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bwana
George Bajuta amewataja watumishi waliosimamishwakazi kuwa ni pamoja na
mweka hazina wa Halmashauri Mazengo Matonya, mhasibu msaidizi Marseli
Siima, mhasibu wa matumizi Wellu Sambalu na afisa mipango wa Halmashauri
hiyo Hamisi Khatimba.
Hata
hivyo Bwana Bajuta ameweka wazi kwamba kwa mujibu wa kanuni,sheria na
taratibu za mikutano ya Halmashauri, mkurugenzi mtendaji ndiye katibu wa
vikao hivyo na kwa kuwa pamoja na kuwa na taarifa ya mkutano huo
hakuweza kuonekana katika ukumbi huo,wajumbe wa mkutano huo walilazimika
kumchagua,afisa kilomo wa wilaya,Paul Lukumai kuwa katibu wao.
Akizungumza
baada ya kuchaguliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya, afisa kilimo wa wilaya hiyo, Paul Lukumai alitaka
kufahamu uteuzi wake ni wa maandishi au wa maneno tu,kwani anachofahamu
yeye wajumbe hao wamemchagua yeye kukaimu na siyo kumteua au kama
mwanasheria ataeleza vinginevyo.
Hata
hivyo mkutano huo maalumu nusura uingie dosari baada ya mkuu wa wilaya
ya Hanang,Bwana Thobiasi Mwilapwa kuingia ukumbini na kutaka kumtetea
Mkurugenzi mtendaji huyo,huku akiwatishia wajumbe wa mkutano huo kwamba
mkutano haukuwa halali.
Ameweka
bayana kwamba kutokana na sababu au mazingira yalivyo au nafasi ilivyo
haikuwezekana kukutana na viongozi hao na ndipo alipofikia uamuzi wa
kwenda kusimama mwenyewe kutoa ujumbe wa serikali akiwa mkuu wa wilaya
kwamba mkutano huo siya halali.
Kikao
hicho kilichotakiwa kuanza majira ya saa nne asubuhi kililazimika
kuanza majira ya saa sita mchana kutoka na wajumbe wa mkutano huo
kumsubiri katibu wa kisheria wa mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji kwa saa mbili bila mafanikio,zaidi ya kumtumia Mkuu wa
wilaya,Thobiasi Mwilapwa ambaye hata hivyo alijikuta akitolewa nje ya
ukumbi huo.
Na Jumbe Ismailly, Hanang
Baadhi
ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Manyara waliohudhuria
mkutano wa kumkataa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo
kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 82 za
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mmoja
wa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Manyara (aliyesimama)
akimnong’ononeza jambo Mwenyekiti wa hiyo,Bwana George Bajuta (wa kwanza
kutoka kulia) kuhusu kuchelewa kufika ukumbini kwa kaimu Mkurugenzi
mtendaji,Bwana Paul Lukumai.
Mkuu
wa wilaya ya Hanang, Manyara, Bwana Thobiasi Mwilapwa akimsikiliza
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo alivyokuwa akimbembeleza kaimu mkurugenzi
kwenda kukaa kwenye nafasi yake.
Mkuu
wa wilaya ya Hanang, Manyara,Bwana Thobiasi Mwilapwa akitoa ufafanuzi
wa kisheria kuhusu mkutano huo kwa waandishi wa habari muda mfupi baada
ya kutolewa nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.(Picha zote na
Jumbe Ismailly)
Muonekano wa jengo la Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Manyara.
Comments
Post a Comment