Fahamu aina saba za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke


Fahamu aina saba za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke na kusababisha maumivu kwao lakini aina hizi saba ndiyo huonekana sana kwa wanawake wengi ambazo ni kama ifuatavyo:
 I. Follicular cyst:
 Ni uvimbe ambao hutokea wakati Ovulation isipotokea au baada ya Corpus Luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya Ovulation. Maumivu haya huonekana kwa robo ya wanawake wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2.Corpus Luteum cyst;
 Ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida Corpus Luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwingine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3. Hemorrhagic cyst:
Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke (kushoto au kulia).

4. Dermoid cyst:
Uvimbe huu ambao siyo saratani na pia hujulikana kama Mature Cystic Teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na Cartilage. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.

5. Polycysitic appearing cyst:
 Uvimbe wa aina hii unakuwa ni mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6. Cystedenoma:
Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za Ovary na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.

7. Endometriomas /Endometrial Cysts:
 Husababishwa na uwepo wa aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama Endometrium kwenye mayai ya mwanamke. Huathiri wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito na huambatana na maumivu sugu ya nyonga wakati wa hedhi. Uvimbe huu unakuwa na damu ya rangi nyekundu inayoelekea kuwa kahawia na ukubwa wake ni kuanzia inchi 0.75 hadi 0.8.

Tiba yake na nini husababisha wiki ijayo, TUPE MAONI YAKO NDUGU MDAU WETU.



Comments

Popular posts from this blog