Updates: Uchaguzi wa Meya Jiji la Dar
Mh. Edward Lowassa na Godbless Lema wakiwasili Ukumbi wa Karimjee kunakofanyika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt
Vincent Mashinji (aliyesimama katikati) na Makamu Katibu Mkuu wa Chadema
Zanzibar, Salum Mwalim (wa kwanza kutosho) na baadhi ya wajumbe wakiwa
nje ya Ukumbi wa Karimjee ambapo wamefika kufuatilia uchaguzi wa Meya wa
Jiji la Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji wa kwanza kushoto akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe.
Maofisa wanaosimamia uchaguzi huo
wakikagua taarifa za wajumbe wanaositahili kuingia ukumbini kwa ajili
ya kumchagua Meya wa Jiji la Dar.
Hali ilivyo ndani ya Ukumbi wa Karimjee ambapo uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam unafanyika.
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, kuamuru uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
kufanyika leo kama ilivyopangwa. Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki
uchaguzi huo wamefika ukumbini Karimjee ambapo uchaguzi huo unafanyika.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji
la Dar es Salaam, Sarah Yohana alitangaza na kutoa barua kwa wajumbe
husika juu ya wito wa kikao cha Baraza la Madiwani kitakachokuwa na
ajenda ya uchaguzi akisema wajumbe 163 watashiriki kupiga kura, kati yao
87 ni kutoka Ukawa na 76 CCM.
Wagombea wanaowania kiti cha Umeya wa Dar ni, Yenga Yusufu Omary (CCM ) na Isaya Mwita Charles (Chadema).
Comments
Post a Comment