Mke, mume wazua timbwili studio za radio
Wakiwa studio. Stori: Dustan Shekidele, Wikienda Morogoro: Kioja! Mwanamke Betina Kimbe (25) na mumewe, Emmanuel Peter (30), wamezua timbwili ‘hevi’ ndani ya Studio za Radio Planet FM ya mjini hapa baada ya mke kukimbilia redioni akiomba achangiwe nauli ya kurudi kwao mkoani lringa akitaka kumtoroka muwewe kwa sababu alimweka ‘bondi’ wakati wa Mechi ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jijini Dar wiki iliyopita. Betina alitinga na mwanaye wa mwaka mmoja ndani ya studio hizo akitokea nyumbani kwa baba mtoto wake huko Dumila kwa madai ya kuchoshwa na mumewe huyo huku akimshushia tuhuma lukuki. MKE ‘AMTUMBUA JIPU’ MUMEWE Akihojiwa na Mtangazaji Warda Makongwa wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM, Betina alisema aliamua ‘kumtumbua jipu’ mumewe huyo kufuatia mateso aliyokuwa akiyapata kila kukicha. “Nilipojifungua mtoto huyu, mume wangu alishinda klabuni, aliporudi nyumbani alikuja na mwanamke na kulala naye chumbani kwetu huku mimi akinilaza chini. “Nilip