Posts

Linah alala na Wizkid hotelini

Image
Mwanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’. Stori: Musa Mateja, Wikienda Dar es Salaam: Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka. Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo. Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’. Kikieleza kwa kujiamini, kiliweka wazi kuwa Linah alilala kitanda kimoja na staa huyo kwenye hoteli moja iliyopo Masaki, Dar, baada ya msanii huyo kutua Bongo kwa ajili ya kufanya makamuzi kwenye moja ya shoo zake alizokuwa ameletwa na promota King Solomon. “Linah alilala na Wizkid, alikaa naye hadi siku anaondoka kulelekea Nigeria, na nikwambie ukweli uliyojificha ni kwamba, Linah ku...

Wabunge wa Upinzani Waingia na Mabomu ya Machozi Bungeni...Wavaa Gas Mask na Kuyalipua...

Image
Hili ni bunge la Kosovo, nchi iliyojipatia uhuru mwaka 2008 baada ya Yugoslavia kusambaratika. Bunge la Kosovo ni bunge linaloongoza kwa vituko barani Ulaya. Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano mkali bungeni kati ya Serikali na wabunge wa upinzani. Hoja kuu ya upinzani ni Serikali itoe ufafanuzi kwanini nchi yao ya Kosovo imekithiri kwa rushwa, ubadhirifu, ukosefu wa ajira na umasikini. Tarehe 19 Februari mwaka huu bila kutarajiwa wabunge wa upinzani waliamua kuingia bungeni huku wakiwa wamejihami kwa kuvaa vifaa vya kuzuia gesi (gas mask) na kuanza kuwarushia wabunge wa chama tawala mabomu ya machozi.

WATU SABA AKIWAMO MTOTO WAUWAWA KWA RISASI MAREKANI

Image
Watu saba wameuwawa kwa kupigwa risasu akiwemo mtoto wa miaka nane huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika tukio la mauaji lililotokea huko Kalamazoo, Michigan nchini Marekani jana usiku. Mkuu wa Usalama wa Umma wa Kalamazoo Jeff Hadley mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa leo asubuhi. Polisi wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwenye gari linaloshabihiana na lililotumiwa mshambuliaji, ambapo pia bunduki ilipatikana kwenye gari hilo. Mtuhumiwa huyo mzungu mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkazi wa kaunti ya Kalamazoo, imeelezwa alijisalimisha bila ya purukushani.

Wasanii wawili wafa Bongo Muvi

Image
Stori: Imelda Mtema, Wikienda Dar es Salaam: Misiba! Wakati wadau wa Bongo Movies wakiwa kwenye majonzi ya kifo cha Michael Dennis ‘John Woka’, kwenye Bongo nako kuna pigo la kuondokewa na wasanii wawili, Maneno Gongo ‘Mr Gongo’ na Jennifer Vincent ‘Mama Utajiju’. Gongo alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa. Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, ndugu wa marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa, alisema kuwa msanii huyo alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda refu na alikuwa akijaribu kila dawa bila mafanikio. Mchuwa alisema kuwa jamaa huyo alizidiwa hadi akakakamaa hivyo walimpeleka Muhimbili ambapo ndiko alikokutwa na umahuti. Msanii huyo ambaye alizikwa kwenye Makaburi ya Visiga, Kibaha mkoani Pwani amecheza filamu mbalimbali zikiwemo The Mask akiwa na Aunt Ezekiel, For Sale, Stolen Gold, Sara na nyinginezo. Wakati simanzi hiyo haijapoa, mwigizaji mwingine, ...

MUHONGO: NCHI INAHITAJI UMEME WA UHAKIKA

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ili Tanzania iwe nchi ya viwanda inahitaji umeme wa uhakika na nafuu. Mara kadhaa, Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana na kukuza uchumi. Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni jana, Profesa Muhongo alisema amewapa kazi Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuangalia namna ya kupunguza bei za umeme. Alisema amewaagiza wadau hao wa nishati kumpa ripoti kamili ya namna ya kupunguza gharama za umeme na vyanzo vya kuzalisha ifikapo Machi mwaka huu. “Lengo ni kuhakikisha tunaangalia namna ya kwenda katika uwekezaji wa viwanda huku kukiwa na umeme nafuu,” alisema. Alisema bei ya umeme haiwezi kupungua kama vyanzo vya kuzalisha umeme havitaongezeka. Alisema mkakati uliopo ni kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambao kwa sasa kuna tani zaidi ya bilioni 10 ambazo...

A-Z Mchungaji Msigwa alivyotaka kuzichapa na DC

Image
   Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa (mwenye koti katikati) akizozana na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela (wa kwanza kutoka kulia). Stori: Mwandishi, Wetu Wikienda IRINGA: Neno zuri linaloweza kutumika ni chupuchupu! Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa nusura azichape na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela kufuatia mchungaji huyo kupandwa na hasira akidai anahujumiwa. Ishu hiyo ilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nduli wilayani Iringa ambapo wawili hao na viongozi wengine walikabidhi mabati kwa watu ambao mapaa ya nyumba zao yaliezuliwa na upepo ulioambatana na mvua. Viongozi wengine wakiongea nao baada ya mzozo huo. Ishu ilianza pale Msigwa alipoonesha kukasirishwa kwa DC huyo kutaka kumuengua kwenye picha ya kukabidhi mabati hayo.Mchungaji Msigwa alimjia juu DC akisema amekuwa akimhujumu kwa siri ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake. Hali ikawa hivi: Msigwa: Ananikos...

KUKAGUA MIRADI YA MAJI YA RUVU JUU NA RUVU CHINI.

Image
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoka ndani ya moja ya tanki baada ya kukagua ukarabati wa matanki matatu eneo la Kimara yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34. Aliyesimama juu ya tanki ni Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan. Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba ya maji eneo la Kiluvya jijini Dar es salaam ili kukamilisha mradi wa ulazaji wa mabomba hayo na kuwahakikishia wakazi wa maeneo ya  Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata maji ya kutosha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akipata maelezo ya mradi wa ukarabati wa matanki matatu ya maji yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34 yaliyopo eneo la Kimara jijini Dar es slaam kutoka kwa Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan (kulia) wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa w...

Mbinu mpya ya Mastaa kujiuza

Image
Masogange Na Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Imevuja! Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa kutosha! Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi. Giggy Money NCHI ZENYE WATEJA WENGI Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini. India ni kwa mbali sana! INAVYOKUWA SASA Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya ‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume wakiwaona wavu...

Talaka ya Jide Mazito Yaibuka!

Image
Mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’. Na Musa Mateja Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ kupewa talaka mahakamani na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’ mazito yameibuka baada ya kubainika uwepo wa hati nyingine ya talaka aliyoitoa Gardner kwa mwanamke mwingine, Risasi limeinasa. Jide Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa mbali ya Jide anayetarajia kuibuka na kishindo kikubwa cha mabadiliko ya muziki wake hivi karibuni, Gardner alimpa talaka mahakamani mkewe wa awali aliyefahamika kwa jina la Idda Pius Mkunja, mwaka 2003. “Mwenzangu Gardner anaonekana ndiyo kamchezo kake kumalizia ndoa mahakamani, ukiachana na Jide nimeona hati ya talaka nyingine aliyoitoa kwa Idda ambaye alimuona mwaka 1997,” kilisema chanzo hicho huku kikimpenyezea hati hiyo ya talaka (tazama pichani) mwanahabari wetu. Siku ya ndoa yao Kama hiyo haitoshi, c...

WAZIRI NAPE AONGEZA HAMASA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.( Picha na: Frank Shija,WHUSM) Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiy...

Things To Never Do With Or In Front Of Your Partner

Image
When you officially (and finally!) become a couple, every second of spending time together is bringing you joy and you having the happiest time of your life. Okay, that’s what all of us are dreaming of. Everything is sweet and lovely for the first few months, but… But things become more and more serious, you may even decide to live together, and that’s when disaster starts. Well, actually men undergo the first few months of this “living together” situation much easier than women. We all understand why: we’re sometimes afraid to do things that can surprise or shock our partner (and make him love you less!). There are a lot of exaggerations manifesting themselves in women’s heads. But certain things can really become some kind of turn-offs and start to ruin your relationship. Maybe you didn’t notice doing some of them before. Check the list now! Okay, first of all, even if you feel you’re best friends with your partner, remember, that this “bro stuff” don’t fully work b...

Yanga Jeuri, Simba Kiburi

Image
Wachezaji wa Yanga, Ngoma (kushoto) na Kamusoko (kulia). Waandishi Wetu, Dar es Salaam DAWA ya Jeuri ni Kiburi, Yanga na Simba leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa zinapambana katika mechi ya Ligi Kuu Bara huku nyuma yake kukiwa na vita kubwa. Awali, Simba ilionekana haitafanya lolote katika Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini muda mfupi baada ya Jackson Mayanja kupewa kazi ya kocha msaidizi akiichukua timu kutoka kwa Dylan Kerr, raia wa Uingereza, mambo yamebadilika. Chini ya Mayanja raia wa Uganda aliyewahi kuinoa Bunamwaya ya nchini kwake, Simba imefanikiwa kushinda mechi sita mfululizo za ligi kuu na moja ya Kombe la FA dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro. Wachezaji wa Ibrahimu Ajibu na Juuko Murshid (kulia) wakishangilia. YANGA JEURI Jeuri ya Yanga ipo zaidi katika fedha, kwanza ilikodi ndege kutoka Dar es Salaam hadi Cuepipe, Mauritius kucheza na Cercle de Joachim katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilishinda bao 1-0. Ndege hiyohiyo ikaipeleka Yanga Zanzibar Jum...

Barua ya Jack Cliff yazua simanzi upya

Image
Video Queen, Jack Cliff. NA Imelda Mtema, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Ikiwa imekatika miaka miwili tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, nchini China, Video Queen, Jack Cliff ameibua simanzi upya baada ya kuandika barua ya wazi kwa Watanzania. Simanzi hiyo iliibuka mwanzoni mwa wiki hii mara baada ya barua hiyo kusomwa redioni na Mtangazaji Millard Ayo ambapo barua hiyo ilieleza kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwaweka sawa wanaosambaza taarifa za uongo zinazomhusu. …Akiwa katika pozi. Katika barua hiyo, ameweka wazi kwamba anajuta kubeba madawa ya kulevya na mwisho wa siku kujikuta akiwa kwenye mikono ya polisi kitu ambacho hakukitegemea kabisa. Anahuzunika, ila pamoja na hayo yote, ameamua kuwaomba msamaha Watanzania wote kwa kile kilichotokea. “Inasikikitisha, Mungu amsaidie atoke jamani maana kama kujuta ameshajuta vya kutosha,” alisema John Jimy, mkazi wa Mwenge Dar. Huku taarifa zikiwa zimetolewa katika vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa mpe...

WAZIRI MKUU ATINGA BANDARI YA TANGA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017.  Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) ……………………………………… WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo kesho (Jumamosi)...