MUHONGO: NCHI INAHITAJI UMEME WA UHAKIKA
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ili Tanzania iwe
nchi ya viwanda inahitaji umeme wa uhakika na nafuu.
Mara
kadhaa, Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana na kukuza uchumi.
Alisema
amewaagiza wadau hao wa nishati kumpa ripoti kamili ya namna ya
kupunguza gharama za umeme na vyanzo vya kuzalisha ifikapo Machi mwaka
huu.
“Lengo ni kuhakikisha tunaangalia namna ya kwenda katika uwekezaji wa viwanda huku kukiwa na umeme nafuu,” alisema.
Alisema bei ya umeme haiwezi kupungua kama vyanzo vya kuzalisha umeme havitaongezeka.
Alisema
mkakati uliopo ni kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambao kwa sasa kuna
tani zaidi ya bilioni 10 ambazo hazijaanza kuzalishwa.
Alivitaja vyanzo vingine kuwa ni nishati jadidifu ya jua, upepo, mawimbi na mabaki ya mimea.
Comments
Post a Comment