Ni vitu vidogo lakini ukivizingatika kila asubuhi utakuwa na furaha siku nzima
Wimbo wa Happy wa Pharrell Williams ulikuwa moja ya nyimbo ninazosikiliza kila ninapo amka asubuhi, kwanini sababu ni siku mpya na nilitaka kuanza na furaha kama jina la nyimbo. Je, wewe unafanya nini cha kwanza unapoamka asubuhi.? Kuna vitu vidogo sana unaweza ukawa unafanya kila siku na ukajisikia mwenye furaha na ukaanza siku yako vizuri Usizime Alarm (kengere). Kuna wakati unahitaji kitu cha kukufanya uamke muda unaopanga wewe asubuhi. Kengere ya simu au saa ya mezani, inapoita wengi wetu sababu ya usingizi mwingi tunaizima na kuendelea na usingizi, kwa dakika chache, ila ni vizuri kama ulipanga kuamka muda huo basi na uamke . panga ratiba yako na uizoe. Tafuta Ujumbe wa kukupa moyo. Kuna wakati tunahitaji mtu wa kutuambia tunaweza,weka chumbani kwako ujumbe mzuri wa kukupa moyo kama “You’re the Best” au unaweza ukaingia Google na kutafuta “inspiration quotes” hizi ni nikuu za watu mbalimbali, ambazo unaweza kusoma kila unapo amka uanze na siku mpya