WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA BAADA YA KUKUTWA WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa mkoani Mbeya. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA. TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2016. KATIKA TUKIO LA KWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU ISMAIL [31] MFANYABIASHARA NA MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO KILO 7 NA GRAMU 100 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA KWENYE MABEGI YA NGUO. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 05:30 ASUBUHI HUKO CUSTOM MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. AIDHA MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA SAFARINI AKITOKEA SOUTH AFRIKA KUELEKEA JIJINI DSM AKIWA NA PASSPORT NO. AB.767234 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 21/10/2015 NA KUSAFIRI KWENYE BASI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 BPR MALI YA KAMPUNI YA FALCON IKITOKEA LUSAK...