WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA BAADA YA KUKUTWA WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2016.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU ISMAIL
[31] MFANYABIASHARA NA MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI
UZITO KILO 7 NA GRAMU 100 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA KWENYE MABEGI YA NGUO.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
18.01.2016 MAJIRA YA SAA 05:30 ASUBUHI HUKO CUSTOM MPAKANI MWA TANZANIA
NA ZAMBIA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
AIDHA MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA
SAFARINI AKITOKEA SOUTH AFRIKA KUELEKEA JIJINI DSM AKIWA NA PASSPORT NO.
AB.767234 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 21/10/2015 NA KUSAFIRI KWENYE BASI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 BPR MALI YA KAMPUNI YA FALCON IKITOKEA
LUSAKA KUELEKEA DSM.
KATIKA TUKIO LA PILI, MTU MMOJA MKAZI
WA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA AITWAYE HAMIS SELEMANI
[30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 3
SAWA NA UZITO WA GRAMU 15 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA MFUKONI MWA SURUALI
YAKE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
18.01.2016 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA
YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
NB: Kny – ina maana kwa niaba ya.
Comments
Post a Comment