Posts

MAGUFULI AHIDI KUFUFUA VIWANDA MKOANI TANGA,KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA

Image
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya leo mjini Tanga.      Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano,jioni ya leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.  Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,ambaye pia ni mgombea Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Mh Ummy Mwalimu akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ili aweze kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.  Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo....

RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA‏

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Ha...

LOWASSA AAHIDI UTENDAJI SPIDI 120

Image
MGOMBEA Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, Edward Lowassa amesema endapo atachaguliwa kuwa rais ataunda serikali isiyokuwa ‘nyoronyoro’. Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, Edward Lowassa. Akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Shule ya Msingi Bunju ‘A’, Lowassa alisema muda umefika kwa wananchi wa Tanzania kufanya mabadiliko. “Naombeni mniteue niwe rais wenu ili mpate maendeleo ambayo hamkuwahi kuyapata kwa kipindi cha miaka zaidi ya hamsini. “Mimi nitaunda serikali isiyokuwa nyoronyoro na inayofanya kazi zake kwa ufanisi na kila mtanzania ataweza kunufaika na rasilimali za nchi yake,” alisema Lowassa aliyehutubia kwa takribani dakika kumi. Alisema endapo atafanikiwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano, serikali yake itafanya kazi kwa spidi ya mwendo kasi wa 120 ...

ANASWA NA KOMBATI ZA KOMANDOO

Image
Kijana  Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi. Na Haruni Sanchawa K IJANA aitwaye Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi kutoa dhamana kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa). Taarifa zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa, kijana huyo amekuwa akizutumia sare hizo kwa matukio tofauti huku akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi hilo. Katika utetezi wake mbele ya askari polisi, Zakaria alikiri kuwa sare hizo si zake na… Kijana  Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi. Na Haruni Sanchawa K IJANA aitwaye Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi kutoa dha...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 08.09.2015

Image
SHARE