ANASWA NA KOMBATI ZA KOMANDOO
Kijana Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi.
Na Haruni Sanchawa
KIJANA aitwaye
Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani,
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la
Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi
kutoa dhamana kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa).
Taarifa zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa, kijana huyo amekuwa
akizutumia sare hizo kwa matukio tofauti huku akijifanya ni mwajiriwa wa
jeshi hilo.
Katika utetezi wake mbele ya askari polisi, Zakaria alikiri kuwa sare hizo si zake na…
Kijana Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi.
Na Haruni Sanchawa
KIJANA aitwaye
Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani,
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la
Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi
kutoa dhamana kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa).
Taarifa
zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa, kijana huyo amekuwa
akizutumia sare hizo kwa matukio tofauti huku akijifanya ni mwajiriwa wa
jeshi hilo.
Katika utetezi wake mbele ya askari
polisi, Zakaria alikiri kuwa sare hizo si zake na kwamba ni za kaka yake
aliyetajwa kwa jina la Anord William ambaye alidai ni mfanyakazi wa
jeshi hilo kikosi cha Komandoo, Morogoro.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu zinasema
kuwa mtu huyo alikamatwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Mkoa wa
Kipolisi Temeke wakati akijaribu kutumia sare hizo kuwashawishi askari
hao wakubalia kumpa dhamana mtu aliyetaka kumdhamini.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa kijana huyo
aligundulika kirahisi kuwa si askari kutokana na vitendo vyake kuanzia
kutembea hata kutoa salamu za kijeshi alishindwa.
Taarifa zinadai kuwa kijana huyo
alipofika kituoni hapo alionekana kutokuwa na muonekano wa kiuaskari
kwani alikuwa hajui taratibu za kijeshi kama vile kutambua nani
anapaswa kupewa saluti au ‘kumkaukia’ hali iliyowashangaza askari
kituoni hapo na kulazimika kumhoji ili kubaini ukweli.
Aidha, chanzo hicho kilisema kutokana
na tukio hilo, mtuhumiwa huyo amehifadhiwa eneo maalum kwa ajili ya
mahojiano zaidi huku taratibu zingine zikifanywa ikiwa ni pamoja na
makachero kwenda Morogoro Kikosi cha Komando kuthibitisha kama askari
aliyetajwa na kijana huyo yupo katika kikosi hicho na kujua ilikuwaje
sare zake zikawa kwa mtuhumiwa.
Comments
Post a Comment