RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia
katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya
mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana
Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa
miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace
George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa
hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt.
Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango
wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu
alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje
baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana
Septemba 6, 2015.
Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko
Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume
aliloumia kwenye msongamano huo
Rais Kikwete akimpa pole
mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake
hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
Rais Kikwete na Mama Salma
Kikwete wakimpa pole mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani
pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo
Rais Kikwete akimpa pole
mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini
hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
"Pole sana...." Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi
Rais Kikwete alitumia wasaa
huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na
majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto
Rais Kikwete alitumia wasaa
huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na
majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza
kwenye mti
Rais Kikwete akimpa pole
mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea
Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa
kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye
Rais Kikwete akitoa mapendekezo
ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache
ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya
kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu
nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni Rais Kikwete aliongea
na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa
yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni
kumalizika.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha
Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano
wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.
(PICHA NA IKULU)
Comments
Post a Comment