Posts

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 1.09.2015

Image

SITTA AMJIBU SUMAYE KUHUSU MABEHEWA MABOVU!

Image
Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Sitta akisisitiza jambo. Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo. Wanahabari wakifuatilia tukio.WAZIRI wa Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, baada ya kuituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.  Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.  Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo. Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Indu...

BIA YA KILIMANJARO YAZIPAMBA SIMBA, YANGA

Image
  Na Bertha Lumala, Dar es Salaam WADHAMINI wakuu wa klabu kongwe nchini, Bia ya Kilimanjaro, leo 'wamezipamba maua' baada ya kuzikabidhi jezi na vifaa vingine vipya vyenye thamani ya Sh. milioni 70 kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaoanza Septemba 12. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, amesema wataendelea kuhakikisha mishahara ya wachezaji wa klabu hizo mbili inalipwa huku wakijivunia kuzinunulia klabu hizo mabasi mawili makubwa kwa ajili ya usafiri wa wachezaji. "Tunaamini timu zote mbili zimesajili vizuri na zitafanya vyema kwenye ligi msimu huu. Yanga imetwaa Ngao ya Jamii na Simba imekuwa ikifanya vizuri katika mechi za kirafiki tangu kuajiriwa kwa kocha mpya," amesema Pamela. Vifaa vilivyokabidhiwa leo kwa wawakilishi wa klabu hizo; Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collins Frisch na Meneja Maso...

DK MAGUFULI AZIDI KUNOGESHA KAMPENI ZA CCM ZA URAIS MKOANI RUVUMA

Image
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi ikiwa ni ishara ya kuwasalimia alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga, Mkoa wa Ruvuma leo, ambapo aliahidi kuboresha kiwanda cha kukoboa kahawa na kujenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay. Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Mbunge wa zamani wa Jimbo la Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwaomba wananchi wa Ruvuma kumpigia kura Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli waqkati wa mkutano wa kampeni wa CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji Mjini Songea, mkoani Ruvuma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi ...