SITTA AMJIBU SUMAYE KUHUSU MABEHEWA MABOVU!
Wanahabari
wakifuatilia tukio.WAZIRI wa Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, baada ya kuituhumu serikali ya Rais
Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi
zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa
ni feki.
Akizungumza
na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote
waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka
sasa baada uchunguzi kukamilika.
Aliongeza
kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi
yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli
(TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.
Aidha
amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni
ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo
watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa
zabuni ilikuwa haina sifa.
Hata
hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo haikuwa na
sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa
kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta
mabehewa.
Viongozi
wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles; Mhasibu
Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper Kisiraga;
na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
(NA DENIS MTIAMA/GPL)
Comments
Post a Comment